Uncategorized

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi hii, Lukaku, QPR, Wilson, Jovic, Vukovic

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji na klabu ya Manchester United, Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 25, anapania kujiunga na Juventus endapo atalazimishwa kuondoka Manchester United. (Sun)

QPR huenda wakahamia uwanja wao mpya wenye uwezo wa kuhimili mashabiki 45,000 kama sehemu ya mradi wa maendeleo uliyogharimu euro milioni 425. (Mail)

Meneja wa Leicester Brendan Rodgers anataka kutumia euro milioni 40 kumjumuisha mshambuliaji wa Bournemouth na England Callum Wilson, 27 katika kikosi chake. (Sun)

Manchester City wanamfuatilia mshambuliaji wa Benfica na Serbia Luka Jovic, ambaye anaichezea Eintracht Frankfurt kwa mkopo. (Mail)

Chelsea ni miongoni mwa vilabu vya ligi ya Primia vinavyomtafuta kiungo wa kati wa Croatia na Maritimo Josip Vukovic, 26. (Talksport)

Luka Jovic

Luka Jovic

Arsenal imemuita nyumbani kipa wake Emiliano Martinez ambaye amekuwa akichezea Reading kwa mkopo.

Emiliano anatarajiwa kuwa mlinda lango wa pili kwasababu hawana uwezo wa kumnunua kipa mwingine kuchukua nafasi ya Petr Cech anayeelekea kustaafu. (Sun)

Emiliano Martinez

Emiliano Martinez

Meneja wa Leeds United David Hockaday anasema alijaribu kumsajili mlinzi wa sasa wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk kutoka Celtic alipokuwa Elland Road, lakini ombi lake lilikatalliwa na mmiliki wa klbu hiyo Massimo Cellino. (Guardian)

Chelsea imewauliza mashabiki wake katika mtandao wa Twitter kupendekeza mchezaji ambaye wanataka asajiliwe na klabu hiyo licha ya marufuku ya usajili wa wachezaji inayowakabili. (Reuters)

Mshambuliaji wa Manchester United James Wilson, 23, anasema kuwa aliamua kuhamia Aberdeen kw amkopo msimu huu ili ”kujiuza”. (ESPN)

James Wilson

James Wilson (wa kwanza kushoto)

Real Madrid inapania kumnunua beki wa kushoto wa Ajax muargentina Nicolas Tagliafico, 26, kuchukua nafasi itakayoachwa wazi na Marcelo. (Tuttosport, via Mirror)

Marcelo ambaye ni nyota wa kimataifa wa Brazil anajiandaa kujiunga na Juventus. (Tuttosport, via AS)

Bora kutoka Jumatano

Manchester United inamfuatilia kiungo wa kati wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic, 30. (Mail)

Juventus haina mpango wa kumrudisha tena mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Gonzalo Higuain katika klabu hiyo mkataba wake wa bure utakapokamilika Chelsea. (Il Corriere di Torino, via Sun)

Gonzalo Higuain

Kipa wa Uhispani David de Gea, 28, anakabiliwa na hatari ya kushuka thamani nje ya Manchester United, licha ya klabu hiyo kuwa tayari kumpatia mkataba mpya wa euro £350,000 kwa wiki. (Evening Standard)

Kipa wa Ajax na Cameroon Andre Onana, 22, yuko katika orodha ya kuwa kipa mpya wa Barcelona endapo Jasper Cillessen, 29, ataondoka klabu hiyo. (El Club de la Mitjanit, via Sport)


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents