Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi hii, Man United yajiondoa kwenye mbio za kumnasa nyota huyu Uingereza, Fernandes, Pogba sokoni

Manchester United imejiondoa katika harakati ya kutaka kumsaini beki wa Leicester na Uingereza Harry Maguire baada ya kuambiwa kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atagharimu £100m. (Mirror)

Harry Maguire

Mkufunzi wa klabu ya Nice nchini Ufaransa Patrick Vieira, 43, Mkufunzi wa klabu ya Rangers Steven Gerrard, 39, kocha wa Manchester City Mikel Arteta, 37, wameorodheshwa miongoni mwa wakufunzi wanaotarajiwa kumrithi Rafael Benitez. (Telegraph)

Raia wa Uhispania Mikel Arteta ameungwa mkono kuchukua ukufunzi wa klabu ya Manchester City wakati kocha Pep Guardiola atakapoondoka katika klabu hiyo. (Evening Standard)

Arteta
Image captionArteta

Mkufunzi wa klabu ya Burnley Sean Dyche pia analengwa na Newcastle lakini the Magpies watalazimika kuwalipa Burnley £10m kama fidia. (Daily Mail)

Manchester United itakutana na ajenti wa kiungo wa kati wa Portugal Bruno Fernandes, 24, ili kujaribu kumrai kuhamia katika klabu hiyo kwa dau la £70m kutoka klabu ya Sporting Lisbon. (O Jogo, via Talksport)

Juventus imeitaka kampuni ya vifaa vya michezo Adidas kuisaidia kifedha ili kuweza kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Corriere dello Sport – in Italian)

Paul Pogba

Manchester City iko katika mzungumzo na Juventus kuhusu usajili wa beki wa kulia wa Ureno Joao Cancelo. (Tuttomercato, via Star)

Kiungo wa kati wa Arsenal na Uruguay Lucas Torreira, 23, anasema kuwa AC Milan haijawasiliana naye kuhusu uhamisho katika klabu hiyo ya Serie A. (Talksport)

Bayern Munich imefanya mazungumzo na Paris St-Germain na ajenti wa mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Mirror)

Ousmane Dembele

Beki wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 19 Sepp van den Berg, anatarajiwa kujiunga na Liverpool kutoka kwa klabu ya PEC Zwolle. (Evening Standard)

Beki wa klabu ya Huddersfield Town na Uingereza Tommy Smith, 27, ananyatiwa na Stoke City pamoja na mabingwa wa ligi ya Uskochi Celtic. (Huddersfield Examiner)

Reading wanamnyatia winga wa Brazil Wenderson Galeno, 21, kwa mkopo kutoka Porto.(Futebol365)

TETESI ZA SOKA JUMATANO

Antoinne Griezmann

Barcelona inakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa na Atletico Madrid Antoine Griezmann kwa dau la £107m baada ya kifungu cha sheria cha uhamisho wake kuanza kufanya kazi tarehe mosi mwezi Julai (Telegraph)

Tottenham inakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Lyon na Ufaransa Tanguy Ndombele, 22, kwa dau litakalovunja rekodi £60m.

Ndombele aliichezea Lyon mechi 34 ,msimu uliopita huku ikifuzu katika mashindano ya ligi ya mabingwa baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu ya jedwali la ligi ya daraja la kwanza.. (Sun)

Tonguy Ndombele

Spurs pia inakaribia kumsaini winga wa klabu ya Leeds United Jack Clarke 18, kwa dau la £8.5m. Clarke aliichezea klabu hiyo mara 22 msimu wa 2018-19. (Sky Sports)

Manchester United wanataka kumsaini mshambuliaji wa Sevilla na Ufaransa Wissam Ben Yedder, 28, na wataathiri kifungu cha sheria cha uhamisho wake cha £35.8m. (ABC de Sevilla)

Manchester United ina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa ,15, Mathis Rayan Cherki anayeichezea klabu ya Lyon na ambaye anazivutia klabu kama vile Real Madrid, Juventus, Barcelona na Bayern Munich. (Telegraph)

Simon Mignolet wa Ubelgiji na LiverpoolHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mlinda lango wa Liverpool na Ubelgiji Simon Mignolet, 31, ananyatiwa na klabu ya Crystal Palace. Mwewe hao wa Uingereza wameandaa dau la £8m kumnunua Mignolet, ambaye amesalia na kandarasi ya miaka miwili .. (Evening Standard)

Hatahivyo klabu hiyo ya Anfield haiko tayari kumuuza Mignolet kwenda Palace to Palace na itamuachilia kipa huyo iwapo kitita hicho kitakubalika. (ESPN)

Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, ambaye alifunga katika ushindi wa Liverpool dhidi ya Tottenham katika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya anasakwa na klabu ya Real Betis, huku klabu hiyo ya Uhispania ikiandaa dau la £10m kumnunua mchezaji huyo wa Ubelgiji . (BeIn Sports – in French)

Mchezaji wa Liverpool Divock Origi kulia

Mshambuliaji wa West Ham na Mexico Javier Hernandez, 31,ana mipango ya kuondoka na kuelekea Uhispania na badala yake wana nyundo hao wameamua kumsajili mshambuliaji wa Uruguay na Celta Vigo Maxi Gomez. (Evening Standard)

Leicester imeshinda harakati za kumsaini beki wa klabu ya Luton na Uingereza James Justin kwa dau la £8m ikiwashinda Aston Villa na mabingwa wa ligi ya Uskochi kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Mirror)

Mlinda lango wa zamani wa Itali Gianluigi Buffon, 41

Mlinda lango wa zamani wa Itali Gianluigi Buffon, 41, yuko katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kurudi katika klabu ya Juventus kutoka PSG ambako alikua katika kandarasi ya mwaka mmoja kama mkurugenzi wa klabu hiyo. (Sky Italia via Football Italia)

Winga wa itali na Roma Stephan El Shaarawy, 26, amekubali kujiunga na klabu ya China ya Shanghai Shenhua kwa dau la £16.11m . (Il Tempo)

James Rodrigues

Napoli huenda ikaanza kuitumia jezi nambari 10 ya aliyekuwa nyota wa Argentina Diego Maradona wakijaribu kumrai mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez kujiunga na timu hiyo. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa klabu ya Reading na Gambia Mo Barrow ananyatiwa na klabu ya Montpellier na Rennes.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye aliwahi kuichezea ya Swansea City player ya Uingereza pia ananyatiwa na klabu kadhaa za Uturuki na sasa anataka kuondoka katika wafalme hao baada ya miaka miwilii (getreading)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents