Burudani ya Michezo Live

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi hii, PSG yaigomea Barcelona kwa Neymar, wengine sokoni 

PSG imekataa ombi la klabu ya Barcelona la kumnunua kwa mkopo wa dau la pauni milioni 137 pamoja na kumpatia kandarasi ya kudumu mshambuliaji wa Brazil Neymar mwenye umri wa miaka 27, na badala yake Mabingwa hao wa ligue 1 wakihitaji dau la pauni milioni 229. (Marca)

Neymar

Manchester United inajipanga kutoa dau la pauni milioni 100 kwaajili ya kumsajili winga wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England, Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 19, lifikapo dirisha la usajili la mwezi Januari (Sun)jadon sancho

Liverpool, Manchester City, Manchester United, Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa klabu kuu barani Ulaya zinazomlenga mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20, ambaye ana thamani ya pauni milioni 91. (Sport1 – in German)

Beki wa Liverpool na raia wa Croatia asiyehitajika sana Dejan Lovren, 30, anaivutia klabu ya Ujerumani ya Bayer Leverkusen baada ya kufeli kupata uhamisho kuelekea Roma. (Bild – in German)

Tottenham imeanza mazungumzo ya kumuuza kiungo wa kati wa Kenya Victor Wanyama, 28, kuelekea klabu ya Bruges kwa dau la £11m.Victor Wanyama

Mshambuliaji wa Ubelgiji Michy Batshuayi, 25, anataka kusalia na kupigania nafasi yake Chelsea lakini ataitazama hali mwezi Januari. (Standard)

Manchester City inachunguza hali ya kiungo wa kati wa Argentina na klabu ya Velez Sarsfield Argentine Thiago Almada, 18, ambaye bado hajaandikisha upya kandarasi yake na klabu hiyo.. (A Bola, via Manchester Evening News)Thiago Almada

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anataka kiungo wa kati wa England Herbie Kane, 20, kushiriki katika mechi yao ya kombe la Carabao Cup na hivyobasi kumaliza matumaini ya Portsmouth, Sunderland na Coventry kumsaini mchezaji huyo kwa mkopo. (Portsmouth News)

Bayern Munich are open to selling former Germany defender Jerome Boateng, 30, for £22m. (Mail via Marca)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW