Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi hii, Tottenham na Juventus kubadilishana wachezaji, N’Golo Kante kutua Madrid

Tottenham huenda ikabadilishana kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27, na mshambuliaji wa Juventus’ raia wa Argentina Paulo Dybala, 25, wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Tuttosport, via Express)

Tottenham huenda ikabadilishana kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen,

Kiungo wa kati wa Manchester Paul Pogba, 26, amekubali malipo ya mahshara wa £429,000 kwa wiki na Paris St-Germain kabla ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho lakini uhamisho huo uligonga mwamba baada ya Neymar kushindwa kuhamia Barcelona. (Calciomercato, via Sun)

Real Madrid na Chelsea wameafikiana makubaliano ya uhamisho wa kiungo N’Golo Kante, 28, ambapo klabu hiyo itaambia klabu hiyo ya Uhispania iwapo watapokea maombi yoyote ya mchezaji huyo wa Ufaransa. (Defensa Central, via Express)N'golo Kante

Mchezaji anayelengwa na Tottenham Bruno Fernandes, 25, huenda akapatikana huku Sporting Lisbon ikiwa tayari kumuuza kiungo huyo wa kati kwa dau la £62m. (A Bola, via Sport Witness)

Kungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 28, angependelea kujiunga na mchezaji mwenzake wa zamani Vincent Kompany katika klabu ya Anderlecht wakati atakapoondoka Manchester City. (Sky Sports)

Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger amefichua kwamba alijaribu kumsaini Jadon Sancho, 19, wakati winga huyo alipokuwa Manchester City kabla ya kuelekea kujiunga na klabu ya Borussia Dortmund. (Express)Arsene Wenger

Mchezaji wa Chelsea aliyepo kwa mkopo Victor Moses, 28, huenda asitie saini mkataba wa kudumu katika klabu ya Fenerbahce, licha ya klabu hiyo ya Uturuki kuwa na fursa ya kumnunua winga huyo wa Nigeria . (Star)

Manchester United huenda ikamruhusu mkufunzi wake Ole Gunnar Solskjaer kumnunua kiungo wa kati katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku bodi ya klabu hiyo ikiweka fedha tayari kupiga jeki kikosi hicho katikati ya msimu.. (Manchester Evening News)

Winga wa zamani wa England Trevor Sinclair anasema kwamba kiwango cha mchezo cha mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling ni kizuri sawa na kile cha Lionel Messi na Cristiano Ronaldo’s. (Talksport)Raheem Sterling

Sterling, 24, anatarajiwa kuorodheshwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa vizuri kibiashara huku kampuni ya Pepsi ikimtumia katika tangazo ambalo yeye ameshirikishwa pamoja na Paul Pogba na Lionel Messi . (Telegraph)

Mshambuliaji wa Uhispania Inaki Williams, 25, amefichua kwamba aliwasiliana na Man United kabla ya kutia saini mkatava mpya na klabu ya Athletic Bilbao. (Cadena Ser, via Independent)

Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson ameonya mashabiki wa klabu hiyo kwamba huenda kukawa na ‘mateso na maumivu ya moyo’ katika uwanja huo wa Selhurst Park msimu huu. (Standard)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents