Burudani ya Michezo Live

Tetesi za soka barani Ulaya, Guardiola kurudi Bayern Munich, mchezaji nyota wa Spurs kuvunja mkataba wake

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anadhaniwa kuwa hana furaha kuwa kaskazini magharibi mwa England na Mhispania huyo amehusishwa na mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich. (Bild – in German)

Image result for Guardiola to return Bayern

Meneja wa Uholanzi Ronald Koeman amesema kuna uwezekano wa yeye kupata kazi Barcelona baada ya michuano ya Euro 2020. (Marca)

Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, anataka kuondoka katika ligi kuu ya Ujerumani, huku viongozi wa ligi ya Premia Liverpool wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa England wa miaka 19. (Mail)

Jadon Sancho

Beki wa kushoto na mlinzi wa safu ya nyuma wa England na Tottenham Hotspur Danny Rose, 29, ameapa kukatiza miezi 18 ya mwisho ya mkataba wake baada ya kuambiwa kuwa hatapewa mkataba mpya. (London Evening Standard)

Spurs inahofia kuwa kiungo wa kati wa Denmark wa miaka 27- Christian Eriksen, Jan Vertonghen, 32 na beki Mbelgiji mwenzake Toby Alderweireld, 30, watafuata hatua sawa na ya Rose na kuondoka kwa uhamisho wa bure mikataba yao itakapokamilika msimu ujao . (Star)Kiungo wa katoi wa Tottenham Christian EriksenKiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen anasema kuwa Spurs inaweza kushinda ligi ya premia msimu huu

Winga wa Chelsea na Brazil Willian, ambaye mkataba wake Stamford Bridge unamaizika msimu ujao, analengwa na Juventus na Barcelona, na huenda wakajaribu kumsaini kiungo huyo wa miaka 31 mwezi Januari wakiafikiana . (Mirror)Willian alifungia Chelsea mabao 13 na kusaidia ufungaji wa mabao 12 msimu uliopitaWillian alifungia Chelsea mabao 13 na kusaidia ufungaji wa mabao 12 msimu uliopita

Arsenal, Liverpool na Manchester United zote zinamfuatilia mshambuliaji wa West Brom wa miaka 16 ambaye pia ni raia wa Uingereza, Jovan Malcolm. (Mirror)

Mchezaji wa Manchester City David Silva, 33, anaelekea kujiunga na Mhispania mwezake wa miaka 35 anayecheza safu ya kati Andres Iniesta katika klabu ya Japani ya Vissel Kobe mkataba wake katika uga wa Etihad utakapokamiliki msimu ujao. (Mail)David SilvaDavid Silva aliichezea Manchester City mechi 50 katika ligi ya mwaka 2018-19, na kufunga mabao 10

Bayern inaonekana kuwa tayari kurejelea mpamngo wa kumsaka Leroy Sane,23, baada ya kuumia goti kwa kiungo huyo kuizua kumsajili msimu wa joto. (Mail)

Napoli huenda ikalazimika kumuuza mlinzi wa Senegal wa miaka 28 Kalidou Koulibaly, amabye amehusishwa na uhamisho wa Manchester United, huku mshambuliaji wa Ubelgiji wa miaka 32 Dries Mertens, akinyatiwa na Arsenal. (Ilmattino – in Italian)Kalidou KoulibalyKiungo wa kati wa kimataifa wa Senegal Kalidou Koulibaly

Arsenal inamfuatilia kiungo wa kati wa Stuttgart wa wachezaji wa chini ya miaka 21 Mbelgiji Orel Mangala, 21. (HLN, via Express)

Mkurugenzi wa michezo wa Juventus Fabio Paratici ameonekana Manchester, huku tetesi zikiashiria kuwa anafuatilia mpango wa kubadilishana wachezaji utakaomhusisha kiungo wa kati wa Manchester United wa miaka 26- Mfaransa Paul Pogba na mashambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic, 33. (talksport)Paul PogbaMkurugenzi wa michezo wa Juventus Fabio Paratici ameonekana Manchester huku kukiwa na tetesi huenda Paul Pogba akajiunga na Juventus

Leicester City inahusishwa na usajili wa mwezi Januari wa mshambuliaji wa Senegal na Metz Habibou Diallo,24. (Leicester Mercury)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW