Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa hii, ndoto za Hazard ni kutimkia Madrid,Man italazimika kuandaa kitita kinono kwa Coutinho, United yatia mguu kwa Fernandes

Nyota wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard anahitaji kutimkia Real Madrid haraka iwezekanavyo licha ya timu hiyo kutokuwa tayari kumuachia mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ubelgiji mwenye umri wa miaka 28 kwa dau lisilopungua chini ya pauni milioni 100. (ESPN)

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard

Manchester United italazimika kulipa euro milioni 100 iwapo wanataka kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho. Mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 ni miongoni mwa mwachezaji 10 ambao wanatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu . (AS – in Spanish)

Bruno Fernandes.

Kocha Mkuu wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola haonyeshi nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa timu ya Sporting Lisbon na Ureno mwenye umri wa miaka 24, Bruno Fernandes. (The Sun)

Hata hivyo Manchester United wameonyesha mpango wa kumuhitaji, Fernandes huku lengo la kocha Mkuu wa United,  Ole Gunnar Solskjaer akitaka kuimarisha safu yake ya kati . (ESPN)

Beki wa Tottenham, Toby Alderweireld amesema kwamba yuko asilimia 100 kwamba atarudi kujiunga na Ajax siku zijazo. Raia huyo wa Ubelgiji ,30, alihudumu katika klabu hiyo ya Uholanzi kutoka 2008 hadi 2013. (Voetbal International via Sky Sports)

Alvaro Morata

Atletico Madrid lazima iamue iwapo italipa dau jingine la Yuro 18m kwa Chelsea ili kumsaini mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata kwa mkopo kwa msimu mmoja zaidi . (AS – in Spanish)

Beki wa Tottenham na Uingereza Danny Rose amesema kuwa ataondoka katika klabu hiyo iwapo fainali ya kombe la mabingwa Ulaya itakuwa mechi yake ya mwisho na Spurs. Rose mwenye umri wa miaka 28 aliongeza kwamba anahisi kwamba atauzwa (Mirror)

Nahodha wa Ajax na beki Matthijs de Ligt, 19, ataelekea Uingereza au Uhispania mwisho wa msimu, kulingana na afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo Edwin van der Sar. Raia huyo wa Uholanzi amehusishwa na uhamisho wa Barcelona. (Sky Sports)

Matthijs de Ligt

Klabu mpya iliopandishwa katika ligi kuu ya Uingereza Sheffield United inamtaka mshambuliaji wa Middlesbrough ,26, raia wa DRC Britt Assombalonga. (Northern Echo)

Beki wa Tottenham, Jan Vertonghen hajulikani iwapo atacheza fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Liverpool. Raia huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 32, alipata jeraha katika mguu wake katika dakika za mwisho za ushindi wa Spurs dhdi ya Ajax (Guardian)

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents