Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa hii, Pogba mipango ya kuonda United ipo pale pale, Sanchez na wengine sokoni

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Ufaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, bado ana hamu kubwa ya kutaka kuondoka Manchester United kuelekea Real Madrid msimu huu wa joto. (Marca)

POgba

Beki wa kati wa England Harry Maguire, mwenye miaka 26, amekataa pendekezo la thamani ya £278,000 kwa wiki kutoka Manchester City badala ya kujiunga na timu hasimu United. (Star)

Meneja wa United, Ole Gunnar Solskjaer amefanya mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham, Christian Eriksen kuhusu uwezekano wa uhamisho kuelekea Old Trafford, hatahivyo mchezaji huyo wa miaka 27alikuwa anataka kusubiria uhamisho kuelekea Uhispania. (Manchester Evening News)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa United na timu ya taifa ya Chile, Alexis Sanchez, aliye na umri wa miaka 30, yupo tayari kwa uhamisho kuelekea Italia , wakati Juventus, Napoli, AC Milan na Inter Milan zote zikiwania kumsajili. (Mirror)sanchez

Sanchez atashinikiza uhamisho kuondoka Old Trafford kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya Septemba 2. (Times)

Kwa upande mwingine, United imeshindwa kupata mnunuzi wa Sanchez- anayepokea malipo ya £560,000 kwa wiki. (Mirror)

Juventus bado inatumai kumuondoa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Argentina, Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, kabla ya muda wa mwisho wa uhamisho Ulaya – licha ya kwamba mabingwa hao wa Italia bado hawajapokea maombi thabiti kwa mchezaji huyo. (Independent)

Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain, Leonardo anasema mchezaji wa kiungo cha mbele wa Brazil, Neymar “amefanya makosa” lakini amesisitiza kuwa mchezaji huyo wa miaka 27 yupo Paris “kwa miaka mitatu”. (RMC)

Kipa wa Stoke City na timu ya taifa ya England Jack Butland, aliye na miaka 26, ataomba uhamisho kujilazimisha kuwa katika mipango ya meneja wa England, Gareth Southgate kwa ajili ya mashindano ya Euro 2020. (Mail)

Timu ya Brazil Flamengo ilmejitoa katika uhamisho wa mshambuliaji Mario Balotelli baada ya mchezaji huyo wa miaka 29 kuitisha mkataba wa thamani ya £4m. (Mail)Balotelli

Napoli imekubali kumsaini winga wa Mexico mwenye miaka 23 Hirving Lozano kutoka timu ya Uholanzi PSV Eindhoven. (Voetbal International)

Napoli imekataa ombi la thamani ya £82m kutoka kwa Manchester United kwa mchezaji wa miaka 28 raia wa Senegal Kalidou Koulibaly kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho England. (Corriere dello Sport, kupitia Calciomercato)

Winga wa Bournemouth Jordon Ibe anasakwa na mabingwa wa Uskotchi, Celtic. Timu ya Napoli Italia, tayari imemuulizia mchezaji huyo wa miaka 23. (Sun)Koulibaly

Manchester United imewapiga marufuku wachezaji kusaini kumbukumbu au autograph kwa mashabiki katika kiingilio cha uwanja wa mazoezi kutokana na masuala ya usalama.(Telegraph)

Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini anasema alitaka kipa wa Liverpool Adrian, mwenye miaka 32, asalie katika klabu hiyo. (Mail)

Bora za siku ya Alhamisi:

Neymar alikuwa mazoezini mwenyewe siku ya Jumatano, ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapouzwa.(Esporte Interactivo, via Mundo Deportivo – in Spanish)Neymar

Kiungo mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 27, anaweza bado kujiunga na PSG ikiwa hatakuwa sehemu ya ofa ya Neymar. (Goal)

Beki wa kati wa Manchester United Victor Lindelof, 25, anajiandaa kusaini mkataba mpya kwa ongezeko la mshahara mbali na pauni 75,000 alizokuwa akipata kwa wiki. (Aftonbladet – in Swedish)

Bayern Munich huenda wakafufua nia yao ya kumnasa winga wa Manchester City, Leroy Sane, ingawa mchezaji huyo, 23, ana jeraha la mguu, litakalo mfanya kuwa nje ya uwanja kwa miezi saba. (Bild – in German)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents