Aisee DSTV!
SwahiliFix

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa hii, Rooney adai Guardiola angeshinda mataji yote kama angeifundisha timu ya Uingereza

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane bado anahitaji kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea N’Golo Kante, 28. (The Athletic, subscription required)

Ngolo Kante

Manchester United wanamchunguza kiungo wa kati wa Leicester City James Maddison kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 msimu ujao. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa zamani wa England Wayne Rooney anaamini Pep Guardiola angeshinda vikombe vyote iwapo angepewa kuifundisha timu ya taifa ya Uingereza. (Manchester Evening News)Pep Guardiola

Liverpool, Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich zinamnyatia kiungo wa kati wa Napoli Fabian Ruiz, 23. (Calciomercato, via Daily Mail)

Nahodha wa zamani wa klabu ya Chelsea John Terry amepigiwa upatu na mkufunzi wa zamani Roberto Di Matteo kuwa mkufunzi wa klabu hiyo katika siku za usoni. (Athletic, via Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Chelsea Willian anaamini timu yake ina uwezo wa kushinda taji msimu huu licha ya mkufunzi mpya Frank Lampard kushika hatamu katika hali ngumu. (Standard)Willian

Manchester United imeandaa kuongeza maradufu mshahara wa Victor Lindelof, 25, na kumpatia kandarasi ya mshahara wa £150,000 kwa wiki. (Sun)

Mkufunzi wa England Gareth Southgate anasema kwamba mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy huenda akarudi katika kikosi cha taifa licha ya kutangaza kustaafu kutoka soka ya kimataifa mwaka uliopita . (Times, subscription required)

Beki wa zamani wa Arsenal Per Mertesacker ametoa wito kwa kiungo wa kati Asrenal Mesut Ozil, 30, kuimarika na kutoa mchango wake kwa klabu hiyo , akisema kwamba ana kipaji ambacho hakina mchezaji mwengine wa Arsenal. (Talksport)Mesut Ozil

Beki wa kulia wa Tottenham Serge Aurier, 26, amekiri kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu huu.. (Football.London)

Winga wa Everton Yannick Bolasie, 30, ambaye kwa sasa yuko katika klabu ya Sporting Lisbon, anatumai kwamba kandarasi yake itafanywa kuwa ya kudumu msimu ujao. (Record, via Sport Witness)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW