Uncategorized

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa hii, Sanchez, De Ligt, Salah, Higuain, Brahimi

Mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Chile Alexis Sanchez, 30, anaweza kurudi Arsenal baada ya kushindwa kufanya vizuri Old Trafford, amesema mchezaji maarufu wa zamani wa klabu ya Arsenal Marc Overmars. (ADN Deportes – in Spanish)

Chelsea wanaamini kuwa wanaweza kumsajili moja kwa moja mshambuliaji raia wa Argentina Gonzalo Higuain, 31, kwa chini ya euro milioni 36 kama walivyokubaliana na Juventus hapo awali. (ESPN)

Everton, Manchester United na Wolves wote wananmnyemelea winga wa Porto na timu ya taifa ya Algeria Yacine Brahimi, 29, ambaye atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu. (Correio da Manha – in Portuguese)

Beki wa Newcastle United raia wa Uingereza Jamaal Lascelles, 25, alikuwa katika rada za Mancherster United ili kusajiliwa mwezi Januari, kabla ya kocha Jose Mourinho kufukuzwa kazi. (ESPN)

Juventus wametoa ofa ya pauni milioni 44 na mshambuliaji wao Paulo Dybala, 25, kwa Liverpool ili wamsajili mshambuliaji hatari Mohammed Salah, 26. (Tuttosport, via Mail)

Mohammed Salah

Chelsea wapo tayari kutoa euro milioni 45 kumsajili mshambuliaji wa Benfica na timu ya taifa ya Serbia Luka Jovic, 21, ambaye yupo kwa mkopo na klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani. (Bild – in German)

Beki wa kati wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, anataka kumfuata Mholanzi mwenzake kiungo Frenkie de Jong, 21, amesema mchezaji mwenzake Andre Onana. (Goal)

Matthijs de Ligt, 19.

Hata hivyo, Barcelona hawawezi kutoka kitita cha pauni milioni 75 ili kumsajili beki huyo, hali inayoifanya Manchester City kuwa katika nafasi nzuri ya kumnyakua De Ligt. (Mail)

Manchester United wanataka wachezaji wao golikipa David de Gea, 28, na mshambuliaji Marcus Rashford, 21, kusaini mikataba mipya kabla ya msimu huu kwisha.(Goal)

Kipa wa Real Madrid Thibaut Courtois, 26, amesema kuwa anatamani kupata fursa ya kucheza tena katika ngazi ya klabu pamoja na mshambuliaji wa Eden Hazard ,28. Wawili hao wanachezea timu ya taifa ya Ubelgiji pamoja na walikuwa wote Chelsea, Hazard anahusishwa na uhamisho kuelekea Madrid kutokea Chelsea. (VTM Nieuws, via FourFourTwo)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents