Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa hii, Wilfried Zaha mambo ya usajili yamuendea kombo Dybala, Pogba sokoni

Kiungo wa kati wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, amepata pigo baada ya uhamisho wake kwenda Everton kutibuka lakini amesisitiza anataka kuondoka Selhurst Park. (Telegraph)

Image result for wilfried zaha in stress

Zaha anahofia amepoteza nafasi ya kuhama kwa kitita kikubwa imepotea baada ya dirisha la uhamisho wa wachezaji kufungwa siku ya Alhamisi. (Mail)

Meneja wa Palace Roy Hodgson alimzuia Zaha kufanya mazoezi siku ya Alhamisi kwa sababu mchezaji huyo ”hakuwa na utulivu wa kiakili” baada ya kuwasilisha barua ya kuomba uhamisho. (Mirror)

Uhamisho wa mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala,25, kutoka Juventus kwenda Tottenham uligonga mwamba kutokana na changamoto zinazohusiana suala la haki ya picha. (ESPN)

Paulo Dybala

Paulo Dybala

Spurs iliomba usaidizi kutoka kwa Juventus kulipa haki ya picha ya Dybala- lakini mabingwa hao wa Italia hawakua wamejiandaa kulipa fedha hizo. (90min)

Tottenham wanaamini walikua na £64m kumnunua Dybala, lakini Juventus hawakutilia maanani wazo hilo kwa sababu walikuwa wanamlenga Romelu Lukaku japo kiungo huyo alikuwa na mpango wa kuhamia Inter Milan. (Telegraph)

Manchester United ilijiondoa katika mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Croatia Mario Mandzukic, 33, baada ya kutoelewana na mabingwa hao wa Italia . (ESPN)

Mario Mandžukić 

Mandzukic ameichezea Croatia mara 89 times tangu mwaka 2007

Real Madrid wanaamini wamemkosa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, baada ya United kutoimarisha safu yake ya kati siku ya mwisho wa uhamisho wa wachezaji.

Klabu hiyo inayoshiriki ligi ya Uhispania maarufu La Liga, badala yake imeelekeza darubini yake kwa mshambuliaji wa Paris St-Germain na nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27. (Marca)

Hofu ya kikosi cha kwanza kitakacho cheza chini ya meneja mpya wa Chelsea Frank Lampard imemfanya beki wa Brazil David Luiz, 32, kushinikiza uhamisho kwenda Arsenal. (Standard)

Neymar Jr. alipojiunga na Paris Saint-Germain

Neymar

Meneja wa Everton Marco Silva alikuwa tayari kuongeza kasi ya katika safu yake ya mashambulizi siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji na alikuwa namlenga winga wa Arsenal Alex Iwobi, 23 , wa Nigeria akimkosa Zaha. (Guardian)

Tottenham walipata pigo baada ya Sporting Lisbon kukataa kupunguza bei ya kiungo wao wa kati Mreno Bruno Fernandes, 24. (Mirror)

Bruno Fernandes

Bruno Fernandes, Kiungo wa kati wa Sporting Lisbon

United ilipuuza nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa rejected Italia Moise Kean kutoka Juventus, kabla ya kiungo huyo wa miaka 19 kujiunga na mahasimu wao Everton. (90min)

Lakini Everton hawakua tayari kufikia ofa ya Manchester United ya kumuuza beki wa Argentina Marcos Rojo. (Sky Sports)

Rojo alighabishwa sana na hatua hiyo baada ya pendekezo lake kuhamia Everton kutibuka. (Mail)

Marcos Rojo

Marcos Roj0 (kulia)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Louis Saha anasema uamuzi wa klabu hiyo kusaini beki wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 30, wakati wa uhamisho wa wachezaji ni “siri ya ajabu”. (MEN)

Tetesi Bora Alhamisi

Azma ya Barcelona kumsajili tena Neymar, 27, inategemea ikiwa klabu hiyo itamuuza Philippe Coutinho ambaye pia ni mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Brazil. (Goal)

Kingo wa kati wa Juventus Sami Khedira, 32, amekataa uwezekano wa uhamisho mara mbili kwa sababu anaazimia kujiunga na Arsenal. (Star)

Sami Khedira

Sami Khedira, kiungo wa kati wa Juventus

Manchester United wako tayari kulipa £81m ambayo itawawezesha kumnyakua mshambuliaji wa Uhispania na Athletic Bilbao Inaki Williams, 25. (El Chiringuito TV – via Mail)

Pendekezo la Leroy Sane kuhamia Bayern Munich kutoka Manchester City limeathiriwa na jeraha la goti linalomkabili nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Mail)

Leroy Sane

Leroy Sane (Kulia)

Atletico Madrid wanajiandaa kumsajili mchezajiwa safu ya kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Independent)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents