Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi hii, Inter kumsajili Lukaku, Madrid kuanza na Pogba kisha kumalizana na Eriksen

Inter Milan wanataka kumsaini mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku, 26, lakini watalazimika kumuuza mshambuliaji wao wa sasa Muargentina Mauro Icardi,26 kufadhili mkataba wa Lukaku. (Guardian)

Real Madrid wanampango wa kumnunua Paul Pogba kutoka Manchester United msimu huu wa joto kabla ya kumsaini mchezaji nyota wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Goal)

Tottenham watamchukua winga wa Uhispania wa miaka 22 Marco Asensio kama sehemu ya makubaliano ya uhamisho wa Eriksen kwenda Madrid . (Sun)

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameiambia klabu hiyo imuuza Pogba kwa klabu itakayoweka dau kubwa zaidi, japo Juventus wameonesha nia ya kutaka kumnunua. (Star)Paul Pogba na Ole Gunnar SolskjaerHaki miliki ya pichaREUTERS

Image captionPaul Pogba na Ole Gunnar Solskjaer

Tottenham inatarajia Juventus itaweka dau la kumnunua beki wa kulia Kieran Trippier, 28, na wako tayari kumuuza kiungo huyo wa kimataifa kwa karibupauni milioni 25. (Telegraph)

Paris St-Germain wameiambia Barcelona kuwa hawamuuzi Neymar, 27 kwa udi na uvumba. (Mail)

Real Madrid wanampango wa kusaini Ian Kylian Mbappe,26 kutoka PSG msimu ujao lakini wanataka mchezaji huyo raia wa Ufaransa kutoa ombi la kutaka uhamisho. (AS)Neymar na Kylian MbappeHaki miliki ya pichaREUTERS

Image captionNeymar (kushoto) na Kylian Mbappe

Atletico Madrid wanamtaka beki wa Arsenal Mhispania Hector Bellerin, 24, na wako tayari kumwachilia winga Vitolo, 29, kama sehemu ya mkataba wa usajili wake. (Telegraph)

Chelsea hawajaamua kumuuza mlinzi wao Mfaransa Kurt Zouma, 24, kwa Everton hadi watakapopata kocha mpya. (Star)

The Blues wanajiandaa kuilipa Derby pauni milioni 4 zinazohitajika kutimiza masharti ya mkataba wa Frank Lampard kabla hawajakamilisha mchakato wa kumuajiri kama kocha wao mpya wiki ijayo. (ESPN)

Chelsea wamempatia kipa Petr Cech la kiufundi na mshauri wa michezo wakiwa na matumaini kuwa atashirikiana kwa karibu na Lampard. (Guardian)Petr CechHaki miliki ya pichaAFP

Image captionPetr Cech

Klabu ya Shanghai Greenland Shenhua kutoka China imetoa ofa ya pauni milioni 17.8 kumnunua Willian, 30, lakini mchezaji huyo wa Brazil huenda asikubali kujiunga nao kwasababu bado anataka kusalia Chelsea. (UOL Esporte, via Metro)

Mpango wa Arsenal wa kumnunua winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco au mshambuliaji wa Bournemouth Ryan na Uskochi Fraser huenda umekwama. (Evening Standard)

Meneja mpya wa Juventus Maurizio Sarri amesema hana mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 27, kutoka Chelsea. (Sun)JorginhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Image captionJorginho
Presentational white space

Tetesi Bora Ijumaa

Juhudi za kocha Ole Gunnar Solskjaer kuimarisha kikosi chake huenda zikagonga mwamba kwa sababu Manchester United ni klabu ambayo hutoa ofa ya chini kwa wachezaji wanaotaka kuwasajili. (Evening Standard)

Solskjaer anataka kumuuza kiungo wa kati wa Man Utd Mfaransa Paul Pogba, 26, bada ya kufahamishwa kuwa ana pauni milioni 100 ya kuwasajili wachezaji wapya msimu huu. (Star)Ole Gunnar SolskjaerHaki miliki ya pichaREUTERS

Image captionOle Gunnar Solskjaer

Mchezaji nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27, hana mpango wa kuchezea tena Paris St-Germain. (Sport – in Spanish)

Real Madrid wameweka dau la euro milioni 130 kumnunua Neymar, kutoka PSG, mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, au mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, 27. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Manchester City wanapigiwa upatu kuipiku Man Utd katika usajili wa Harry Maguire, 26, kutoka Leicester kwa kima cha pauni milioni 65 baada ya kiungo huyo wa England kupita vipimo vya matibabu. (Star)Harry MaguireHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Mhispania Rodri, ameamua kujiunga na Man City badala ya Bayern Munich na kuhamia City kawa malipo ua £62m. (Kicker – in German)

Everton wameanza maungumzo na Chelsea kuhusu usajili wa Kurt Zouma kwa mkataba wa kudumu baada ya mlinzi huyo wa Ufaransa, 24, kucheza Goodison Park msimu uliopita kwa mkopo katika. (Telegraph)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents