DStv Inogilee!

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi hii Zidane, Rakitic, Holland, Ospina, Rabiot

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane hatazuiliwa na marufuku ya usajili ya Chelsea kuwa meneja mpya katika uga wa Stamford Bridge.

Huenda akatumia euro milioni £200 wakati wa rufaa ya The Blues. (The Sun)

Ama Chelsea huenda wamchukuwa naibu meneja wa EnglandSteve Holland ikiwa watamfuta kocha mkuu Maurizio Sarri wiki ijayo. (Daily Telegraph)

Ivan Rakitic

Vilabu vingine vinne vya lligi ya primia vinakabiliwa na hatari ya kupigwa marufuku ya usajili kwa kukiuka sheria ya kuwasajili wachezaji wadogo. (Daily Mail)

Chelsea watakabiliwa na ushindani kutoka kwa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich katika juhudi zao za kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona, mcroatia Ivan Rakitic, 30. (The Sun)

Arsenal wamempatia kazi ya mkurugenzi wa kiufundi wa Roma Monchi.

Raia huyo wa Uhispania wa miaka 50 aliwahi kufanya kazi na meneja wa Arsenal Unai Emery akiwa Sevilla ambako alitengeneza jina kwa kuwasajili wachezaji kama vile Dani Alves na Ivan Rakitic.(Mirror)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 23 anayechezea Paris St-Germain, anapigiwa upatu kujiunga na Tottenham au Liverpool, baada ya ajenti kukosa kujiunga na Barcelona. (Sport, via Talksport)

Adrien Rabiot

Napoli wanakaribia kumsajili kipa wa Arsenal na Colombia David Ospina, 30. (Calciomercato)

Milan Skriniar wa Inter Milan anakaribia kutia saini mkataba mpya na klabu hiyo.

Beki huyo wa kati raia wa Slovakia anadiwa kulengwa na Manchester United. (Sky Italia via Calciomercato)

Mwenyekiti wa PSG Nasser Al-Khelaifi amesema kuwa klabu hiyo haitalazimishwa kuwauza Neymar, 27, na Kylian Mbappe, 20, kwasababu ya masharti ya Uefa ya usawa wa kifedha. (ESPN)

Kylian Mbappe

Bayern Munich wanatarajiwa kiumsaini mshambuliaji wa kimatifa wa Ivory Coast Nicolas Pepe,23, anayechezea Lille.

Arsenal, PSG na Barcelona pia wanamezea mate nyota huyo ambaye ameifungia klabu yake ya Ufaransa mabao 16 msimu huu. (Le10 Sport in French)

Everton wanatafakari uwezekano wa kumsajili beki wa kulia wa PSG Thomas Meunier, 27.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amecheza katika kikosi cha kwanza cha mechi 13 za PSG msimu huu. (Le10 Sport, via Sun)

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW