Uncategorized

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne hii, Herrera asaini makubalino ya awali na PSG, Keane, Costa, Fraser, Ake, Martinelli

Kiungo wa Manchester United Ander Herrera mwenye umri wa miaka 29, amesaini makubaliano ya awali na klabu ya Paris St-Germain ili ajiunge na miamba hiyo ya Ufaransa mwishoni mwa msimu. (Daily Record)

Ander Herrera

Manchester United wamegoma kumuongezea mshahara Herrera licha ya kujua kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kumpoteza kiungo huyo raia wa Uhispania bure ifikapo mwisho wa msimu. (Telegraph)

Tottenham wanaweza kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kutoa kitita cha pauni milioni 50 ili kumsajili beki wa Everton raia wa Uingereza Michael Keane, 26, ambaye amekuwa pia akinyemelewa na Arsenal.(Express)

Tottenham pia wamejitosa kwenye mbio za kumsaini mshambuliaji wa Juventus Douglas Costa mwishoni mwa msimu. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 pia anafuatiliwa na na vilabu vya Manchester United na Manchester City, wakati Chelsea na Paris St-Germain hapo awali walikuwa wakihusishwa na mshambuliaji huyo raia wa Brazil. (Tuttosport, via Metro)

Arsenal wanamtazamia winger wa klabu ya Bournemouth Ryan Fraser, 25, kama kipaumbele katika mipango yao ya usajili mwishoni mwa msimu. (Mirror)

Ryan Fraser

Klabu ya Arsenal pia ipo katika mazungumzo na klabu ya Brazil ya Ituano kwa usajili wa kitita cha pauni 6.5 milioni kwa winga kinda wa miaka 17 Gabriel Martinelli, ambaye amekuwa akifuatiliwa na vilabu vikubwa 20 vya balani Ulaya na hivi karibuni alifanya majaribio na Manchester United. (Sun)

Kiungo wa zamani wa Manchester City Yaya Toure, 35, amevishutumu vyombo vinavyosimamia mpira wa miguu kwa kufeli kuwalinda wachezaji weusi dhidi ya ubaguzi. (Mirror)

Yaya Toure

Kocha wa Leicester Brendan Rodgers anatazamiwa kufanya mazungumzo juu ya mustakabali wa kiungo Andy King, 30, klabuni hapo. (Leicester Mercury)

Kocha Bournemouth Eddie Howe amepuuzilia mbali tetesi kuwa klabu za Tottenham na Manchester United zinataka kumsajili beki wake Nathan Ake, 24.(Bournemouth Daily Echo)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents