Aisee DSTV!

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne hii, Madrid kudunduliza fedha za kumng’oa Pogba Man United, Atletico kumuazibu, Griezmann 

Real Madrid inafikiri kumuuza mshambuliaji wake raia wa Colombia James Rodriguez, 27, ili kukusanya £150m kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 26. (Mail)

Tokeo la picha la Paul pogba to Real

Atletico Madrid imeanzisha mchakato wa kumuadhibu mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28, ambaye anatarajiwa kuhamia Barcelona kwa dau la £107.5m . (Guardian)

Napoli ina hamu ya kumsaini James kutoka Real Madrid, pamoja na mshambuliaji wa Argentina na Inter Milan Mauro Icardi, 26. (Goal.com)

Bayern Munich inataraji winga wa Ujerumani Leroy Sane, 23, kuamua wiki ijayo iwapo anataka kujiunga na wababe hao wa Ujerumani kutoka Manchester City. (Mail)Leroy Sane

Arsenal, Manchester United na Paris St-Germain wana hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24, kutoka Chelsea. (RMC Sport – in French)

West Ham wanafikiria kulipa dau la £43.5m na kuishinda Valencia ili kumsajili mshambuliaji wa Celta Vigo na Uruguay 22. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Manchester United na Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, anatumai kuwa mchezaji wa Inter Milan kufikia wakati ambapo ataikabilia Man United tarehe 20 mwezi Julai.. (Mirror)Lukaku

Aston Villa wamewasilisha ofa ya dau la £7m kumnunua kipa wa Burnley na Uingereza Tom Heaton, 33. (Sun)

Arsenal inakaribia kumsajili beki wa Saint-Etienne William Saliba, huku mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 8 akidaiwa kugharimu £25m. (Evening Standard)

Beki wa kushoto wa Liverpool, 27, raia wa Uhispania Alberto Moreno anakaribia kuhamia Villarreal. (ESPN)Gareth Bale

Gareth Bale alikuwepo wakati wachezaji wa Real Madrid waliporudi katika maandalizi ya msimu mpya siku ya Jumatatu , baada ya wachache kutomtarajia mshambuliaji huyo katika timu hiyo. (Marca).

Manchester City inakaribia kumsaini kinda wa Uingereza anayechezea timu ya Uingereza ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 Morgan Rogers kutoka West Brom, (Mail)

Everton inakaribia kuwasilisha ofa ya dau la £35m kumnunua mshambuliaji wa Barcelona na Brazil Malcom.Malcolm

Arsenal pia inamnyatia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (RMC Sport – in French)

Watford ina hamu ya kumsajili winga wa Ufaransa Allan Saint-Maximin, 22, kutoka klabu ya Nice kwa dau la rekodi la £25m. (Sky Sports)

Aston Villa ina hamu ya kusalia kwa mkopo beki wa Man United Axel Tuanzebe baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kuhudumu msimu wake uliopita akichezea klabu hiyo. (Telegraph)

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW