Aisee DSTV!
SwahiliFix

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne hii, Oblak, Pogba, Wan-Bissaka, Rose, Sakai, Kruse, De Ligt

Mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak anataka kuondoka katika timu hiyo msimu ujao na Mslovenia ,huyo mwenye umri wa miaka 26, anapendela kwenda Manchester United zaidi ya Paris St-Germain. (ESPN)

United wako tayari kuongeza £50m kwa ajili ya Wan-Bissaka

Manchester United wameiambia Real Madrid kwamba kiungo wa kati Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, hauzwi na wamekataa kutangaza bei ya mchezaji huyo Mfaransa. (AS)

Juventus wana nia ya kusaini tena mkataba na Pogba, lakini timu hiyo ya championi upande wa Serie A itatakiwa kuwauza wachezaji watano ili kuweza kummudu kiungo huyo wa kati wa United (Mail)

Manchester United wamekuwa wakishauriwa wamchukue Muingereza Wan-Bissaka Aaron anayecheza safu ya kulia-nyuma – licha ya dau la awali kwa ajili ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 21- kukataliwa na Crystal Palace. (Evening Standard)

Manchester United wameiambia Real Madrid kwamba Paul Pogba, hauzwi na wamekataa kutangaza bei ya mchezaji huyo Mfaransa
Manchester United wameiambia Real Madrid kwamba Paul Pogba , hauzwi na wamekataa kutangaza bei ya mchezaji huyo Mfaransa

United wako tayari kuongeza £50m kwa ajili ya Wan-Bissaka. (Mirror)

Manchester United huenda watathmini upya nia yao ya kusaini mkataba na mlinzi wa Tottenham Danny Rose, mwenye umri wa miaka 28, baada ya mchezaji huyo wa safu ya nyuma ya England kukiri kuwa anaweza kuondoka katika kikosi cha Spurs msimu huu. (Manchester Evening News)

Tottenham wako makini na kiungo wa nyuma kulia wa Marseille Mjapani Hiroki Sakai, ambaye ana umri wa miaka 29. (Sky Sports)

Liverpool wameamua kuachana na azma yao ya kusaini mkataba na Werder Bremen-mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ujerumani Max Kruse, mwenye umri wa miaka 31. (Liverpool Echo)

Tottenham wako makini na kiungo wa nyuma kulia wa Marseille Mjapani Hiroki SakaiTottenham wako makini na kiungo wa nyuma kulia wa Marseille Mjapani Hiroki Sakai

Barcelona wako tayari kutupa karata yao ya mwisho katika juhudi za kusaini mkataba na kiungo wa kati -nyuma wa Ajax na Uholanzi Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 19, wiki hii kwa kuanzisha upya mazungumzo na wakala wake Mino Raiola. (ESPN)

Paris St-Germain wanasema wanamatumaini makubwa ya kufikia makubaliano na Ajax kwa ajili ya kuleta kikosini De Ligt. (Mail)

Manchester City na Bayern Munich wanamlenga Rodri, mwenye umri wa miaka 22, ambaye amekwishaamua kuondoka Atletico Madrid, na amesema watamlipa malipo sawa na anayolipwa kiungo yeyote wa kati wa Uhispania anayopokea anapopokelewa kutoka timu nyingine. (AS – in Spanish)

Mchezaji wa safu ya kati wa Ajax na Uholanzi Donny van de Beek, mwenye umri wa miaka 22, “ana malengo ya Primia Ligi ” na angependa kujiunga ima na Manchester United au Tottenham msimu huu. (Talksport)

Manchester City na Bayern Munich wanamlenga RodriManchester City na Bayern Munich wanamlenga Rodri

Valencia wanamtaka mshambuliaji wa Newcastle Muhispania Ayoze Perez, mwenye umri wa miaka 25. (Cope – in Spanish)

Chelsea wamefikiria kwa mara nyingine kusaini mkataba na MCroasia anayecheza safu ya kati Mateo Kovacic, mwenye umri wa miaka 25, kwa mkataba wa kudumu na kutoka Real Madrid. (Evening Standard)

Meneja wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps amefichua katika mkutano wa taarifa za kabla ya mechi kuwa mchezaji wa safu ya nyuma kushoto wa Lyon Ferland Mendy, mwenye umri wa miaka 24, atajiunga na Real Madrid msimu huu. (Marca)

Meneja wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps amesema Ferland Mendy wa Lyon atajiunga na Real Madrid msimu huu
Meneja wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps amesema Ferland Mendy wa Lyon atajiunga na Real Madrid msimu huu

Mchezaji wa safu ya nyuma kulia Nelson Semedo, mwenye umri wa 25, anaweza kuondoka Barcelonamsimu huu, huku Atletico Madrid wakimsaka, lakini klabu ya Catalonia inamtaka kwa bei ya kati ya Euro milioni 45 na milioni 50 mchezaji huyo (Marca)

Manchester wanakaribia kusaini mkataba na mshambuliani ya Kaunti ya Derby-Liam Delap, mwenye umri wa miaka 16- mtoto wake kiungo wa kati wa zamani wa Stoke Rory Delap. (Derby Telegraph)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW