Aisee DSTV!

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano hii Barca wamsajili Griezmann, Madrid yahamia kwa Pogba, Ole Gunnar Solskjaer atishia kuuza nusu ya kikosi chake kisa Cardiff City 

Barcelona wameamua kumsajili mshambuliaji Antoine Griezmann ambaye ametangaza kuondoka kwake Atletico Madrid msimu huu wa joto.

Related image

Hii ni baada ya klabu hiyo ya Uhispania kuondolewa katika kinyang’anyiro cha ubingwa wa Ulaya na Liverpool(Marca)

Real Madrid wameonesha nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26, huku United ikiwa tayari kumuuza mchezaji huyo kwa pauni milioni 150. (Independent)

Licha ya tetesi kuwa Real Madrid wamekubali makataba wa pauni milioni £86 kumnunua Eden Hazard, 28, Chealsea bado wanashikilia kuwa hatamuachilia kiungo huyo hadi walipwe pauni milioni 100.(Evening Standard)

Eden Hazard

Hazard ameambia vyombo vya habari kuwa aliamua kuingilia kati suala hilo na kwamba atajaribu kuishawishi Chelsea kuafikiana na Real kuhusu uhamisho. (Express)

Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ametishia kuuza nusu ya kikosi chake baada ya kushindwa na Cardiff. (Sun)

Bayern Munich wameanza mazungumzo na Manchester City kuhusu uhamisho wa winga wa miaka 23 wa Ujerumani Leroy Sane. (Daily Record)

Mshambuliaji wa Wales, Gareth Bale, 29, huenda asirejea Tottenham kwasababu hana haraka ya kuondoka Real Madrid, kwasababu amesalia na miaka mitatu katika mkataba wake wa £600,000-kwa wiki. (Mirror)Gareth Bale

Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 23, hatauzwa na Manchester United msimu huu kwasababu amemvutia mmoja wa mwenyekiti mwenza Joel Glazer. (ESPN)

Everton wanatafakatri uwezekano wa kumtuma mlinzi wa England wa chini ya miaka 21 Jonjoe Kenny, 22, kwa mkopo msimu ujao, huku Seamus Coleman akitarajiwa kuwa beki wa kulia na safu ya nyuma. (Liverpool Echo)

Manchester United huenda wakatumia pauni £12m kumruhusu mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez ajiunge na Inter Milan kwa mkopo msomaji ujao. (Mirror)Alexis Sanchez

Leicester wanajaribu mpango wa kumrudisha kiungo wa kati wa 22 Mbelgiji Youri Tielemans amabe yuko Monaco kwa mkopo, kwasababu Manchester United na Tottenham wameonesha nia ya kutaka kumnua. (Sky Sports)

Barcelona wanataka kumuuza kiungo mkabaji wa kati Philippe Coutinho, 26, msimu huu wa joto lakini hawatamuachilia aondoke kwa kitita cha euro milioni 100 sawa na (£86.8m). (Sport)Kalidou Koulibably

Manchester United wamerudi nyuma katika mpango wao wa kumnunua Kalidou Koulibably, 27,baada ya kuitisha pauni £90.(Independent)

Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Manchester City wana mpango wa kuwanunua walau wachezaji watatu wapya msimu huu wa joto, huku wakilenga zaidi mlinzi wa safu ya kati na mashambuliaji. (ESPN)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW