Soka saa 24!

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano hii, Perisic, Sarri, Hazard, Buffon, Nani, Jovic, Bale

Real Madrid wanaamini wakati mgumu anaopitia kocha wa Chelsea Maurizio Sarri utawarahisishia kumsajili kiungo Mbelgiji Eden Hazard, 28, mwishoni mwa msimu. (Mirror)

Chelsea wanata kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuchukua nafasi ya Sarri ambaye amekuwa akisuasua. (Sun)

Gianluigi Buffon

Real Madrid wataminyana Barcelona kumsajili streka wa Benfica Luka Jovic, 21, kwa kutangaza dau la euro milioni 45 kwa nyota huyo anayechezea kwa mkopo klabu ya Eintracht Frankfurt. (Bild – in German)

Zinedine Zidane

Wawakilishi wa mchezaji wa Everton raia wa Brazil Richarlison, 21, wamefanya mazungumzo na hav Atletico Madrid kuhusu mshambuliaji huyo kuhamia vigogo hivyo vya Uhispania. (AS – in Spanish)

Kiungo Mjerumani wa Arsenal Mesut Ozil amekuwa akipigiwa chapuo katika vilabu vingine na wawakilishi wake, huku mustakabali wake dimbani Emirates ukibaki kuwa wa mashaka. (Telegraph)

Mesut Ozil

Beki wa kulia wa Crystal Palace Muingereza Aaron Wan-Bissaka anatakia na klabu ya Borussia Dortmund. Mchezaji huyo mwenye miaka 21 pia anatakiwa na Manchester City. (Sun)

Tottenham inataraji kumsajili winga wa Inter Milan na timu ya taifa ya Croatia Ivan Perisic, 30, ambaye alikuwa aknyemelewa na Arsenal mwezi Januari. (Tuttosport, via Football Italia)

Ivan Perisic

Mchezaji wa zamani wa Manchester United raia wa Ureno Luis Nani, 32, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Sporting CP, ananyemelewa na klabu ya Ligi ya Marekani MLS side Orlando City. (Marca – in Spanish)

Winga raia wa Wales Gareth Bale, 29, anaongea kwa ishara tu na wachezaji wenzake wa Real Madrid kwa kuwa bado hajajifunza Kihispania, amesema mchezaji mwenzake Marcelo. (Marca)

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW