Burudani ya Michezo Live

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano hii, Petr Cech kurejea Chelsea, De Gea, Pogba, Zaha, Gomes sokoni

Kipa wa Arsenal mwenye umri wa miaka 37, Petr Cech atarejea Chelsea msimu huu wa joto kuchukua wadhifa wa mkurugenzi wa michezo. (Sky Sports)

Petr Cech

Gunners wanatafakari uwezekano wa kumsajili kwa uhamisho wa bila malipo kipa wa Dynamo Dresden na Ujerumani wa timu ya wachezaji wa chini ya miaka 21 Markus Schubert, 20, msimu ujao kuchukua nafasi ya Cech. (Bild – in German)

Manchester United wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsaini winga wa Swansea na Wales, Daniel James, 21 kwa pauni milioni kumi na tano.(Mail)

United watalazimika kulipa pauni milioni hamsini (£50m) kumpata beki wa Crystal Palace Mwingereza Aaron Wan-Bissaka, 21, ambaye ni meneja Ole Gunnar Solskjaer amemteua kama mchezaji bora atakaye dhiditi safu ya nyuma ya timu yake msimu ujao. (Mirror)

Kipa wa Uhispania na Manchester United David de Gea, 28,amekataa kutia saini mkataba mpya na klabu hiyo wakati mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kukamilika mwisho wa msimu ujao. (Sun)David de Gea

David de Gea

Newcastle na West Ham wanapani akumsajili mshambuliaji wa klabu ya Brugge Mbrazil Wesley Moraes, 22. (Mirror)

Meneja wa Chelsea, Maurizio Sarri, 60, analengwa na Juventus wanapomtafuta nani atakaechukua nafasi ya Massimiliano Allegri huku Mtaliano huo pia akinyatiwa na klabu ya Roma. (Sky Sports)

The Blues hawatazuia Sarri kuondoka ikiwa Juventus itakuwa tayari kulipa hadi pauni milioni tano (£5m) kama fidia ya kumrudisha Italia. (Telegraph)Maurizio Sarri

Maurizio Sarri

Tottenham wamekomesha mpango wao wa kumsajili winga wa Crystal Palace Wilfied Zaha, 26, baada ya kushindwa kufikia bei ya pauni milioni mia moja (£100m) kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast . (Evening Standard)

Spurs hata hivyo wamefanya mazungumzo ya kumsaini mshambuliaji wa Celta Vigo raia wa Uruguay Maxi Gomez, 22, ambaye mkataba wake unamruhusu kuondoka kwa euro milioni arubaini na tatu(£43m). (Star)

Kiungo wa kati wa United Paul Pogba, 26, atapewa jukumu la unahodha wa klabu hiyo katika juhudi za kumshawishi Mfaransa huyo asiondoke Old Trafford. (ESPN)Paul Pogba

Paul Pogba(Kushoto)

Antonio Conte ameshinda makabiliano ya kisheria dhidi ya Chelsea na the Blues sasa ni lazima wamlipe meneja wao wa zamani £9m kama fidia ya kumfuta kazi msimu uliyopita. (Times – subscription required)

Meneja wa Derby County Frank Lampard atajaribu kumsajili mchezji mwenza wake wa zamani katika klabu Chelsea Gary Cahill ikiwa the Rams watainyuka Aston Villa katika mechi ya champions Jumatatu ijayo ili wapandishwe daraja ya kujiunga na ligi kuu ya England msimu wa mwaka 2018-19. (Mirror)

Tetesi Bora Jumanne

Bayern Munich wanaamini kuwa watamsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ujarumani Leroy Sane, 23, kutoka Manchester City msimu huu wa joto. (Mirror)

Chelsea wanatarajiwa kuthibitisha kuwa mshambuliaji wa kimataifa Ufaransa Olivier Giroud, 32, amekubali kusalia katika klabu hiyo kwa mwaka mmoja mwingine. (London Evening Standard)Leroy Sane

Leroy Sane( Aliyevalia jezi nyeupe)

Manchester United wanatarajiwa kuitisha euro milioni 160 (£138m) kumuuza kiungo wa kati wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba, 26. (Star)

Meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ameafiki masharti ya kujiunga na Inter Milan kama kocha wao mpya msimu ujao. (Guardian)

Mlinzi wa Leicester na nyota wa kimataifa wa England Harry Maguire, 26, ni mmoja wa walinzi wa kati wanaolengwa na Manchester City kuchukua nafasi ya Vincent Kompany. (Sky Sports)Harry Maguire

Harry Maguire

Juventus wameachana na Conte na sasa wanamlenga meneja wa sasa wa Chelsea, Maurizio Sarri. (Sun)

Arsenal wametoa ofa ya kumnunua kipa wa valencia Mbrazili Norberto Murara, baada ya kuzungumzana wawakilishi wa mchezaji huyo wa miaka 29. (Star)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW