Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano hii, Pogba, De Ligt, Silva, Chilwell, Sessegnon

Real Madrid haijajiandaa kumlipa mshahara wa pauni 290,000 kwa wiki kiungo wa Man United Paul Pogba iwapo ataka jiunga na miamba hiyo ya Uhispania. (ESPN)

Paul Pogba

Beki wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, anataka kujiunga na mwenzake Frenkie de Jong katika klabu ya at Barcelona msimu ujao lakini Ajenti Mino Raiola angependelea mchezaji huyo kujiunga na Man United , Juventus ama Bayern Munich. (Mundo Deportivo)Kiungo wa kati wa Manchester City Bernardo Silva

Kiungo wa kati wa Manchester City Bernardo Silva, 24, anasema kwamba hajafikiria kuondoka katika ligi ya Premia , licha ya ripoti zinazomuhusisha na mabingwa wa Uhispania Barcelona. (Manchester Evening News)

Arsenal wameambiwa watalazimika kulipa kitita cha £17.2m ili kumsaini mshambuliaji wa PSG ,21, Christopher Nkunku . (Evening Standard)

Manchester City haitamwania beki wa kushoto wa Leicester City na Uingereza Ben Chilwell, 22, kwa sababu wanawamiliki wachezaji mbadala Benjamin Mendy na Oleksandr Zinchenko. (Manchester Evening News)Tottenham wanaongoza harakati za kumsajili kijana wa Fulham Ryan Sessegnon

Tottenham wanaongoza harakati za kumsajili kijana wa Fulham Ryan Sessegnon, ambaye pia anazivutia klabu za Paris St-Germain, Juventus na Borussia Dortmund baada ya klabu hiyo kushushwa daraja kutoka ligi ya Premia. (Evening Standard)

Inter Milan inajianda kumnunua beki wa Man United Matteo Darmian, 29, kurudi Itali , huku klabu hiyo ya Uingereza ikiwa tayari kumuachilia kwa chini ya dau la £9m. (Gazzetta dello Sport, via the Sun)

Kiungo wa kati wa Chelsea aliyeko katika mkopo katika klabu ya AC Milan Tiemoue Bakayoko, 24, anataka kurudi katika uwanja wa Stamford Bridge – na kutoongeza kandarasi yake na mabingwa hao wa Setrie A baada ya kurushiwa maneno ya kibaguzi nchini Itali. (La Republicca, via the Sun)Kiungo wa kati wa Chelsea aliyeko katika mkopo katika klabu ya AC Tiemoue Bakayoko,

Mkufunzi wa klabu ya Rangers Steven Gerrard anamtaka mshambuliaji wa Watford Andre Gray, 27, kuongoza kikosi chake kuwania taji la ligi ya uskochi msimu ujao na klabu hiyo ya ibrox itajaribu kumnunua kwa mkopo. (The Herald)

Mkufunzi wa West Ham Mauricio Pellegrini amemtaja beki wa kati wa klabu ya Alaves Guillermo Maripan, 24, na beki wa kushoto wa Olympiakos Leonardo Koutris, 23, kama mchezaji wanayemlenga kuimarisha safu ya ulinzi (Football.London)Beki wa Crystal Palace Mamadou Sakho, 29,

Beki wa Crystal Palace Mamadou Sakho, 29, amesema kuwa huenda akaondoka katika klabu hiyo baada ya kusema kwamba anataka kucheza soka ya vilabu bingwa Ulaya(Telefoot, via Croydon Guardian)

Newcastle inataka kumsaini mshambuliaji wa Venezuela mwenye umri wa miaka 19 Jan Carlos Hurtado – ambaye amepokea sifa kutoka kwa mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Faustino Asprilla – kutoka kwa timu ya Argentina Gimnasia. (Newcastle Chronicle)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents