Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu hii, Barcelona yaachana na mpango wa Neymar, Madrid yapata mbadala wa Pogba 

Barcelona imefutilia mbali uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wao wa zamani Neymar, 27, kutoka Paris St-Germain katika dirisha hili la usajili. (Goal.com)

Neymar

Manchester United wameafikiana kwa mkataba wa usajili wa mwaka mmoja wenye thamani ya pauni milioni 6.2 na mshambuliaji wa Juventus Mario Mandzukic, 33.

Nyota huyo wa kimataifa wa Croatia huenda pia akafikia gharama ya karibu £15m au atakuwa sehemu ya makubaliano ya kubadilishana na mshambuliaji wa United na Ubelgiji, Romelu Lukaku, 26. (Mail)

Romelu Lukaku

Romelu Lukaku aliifungia United Mabao 15 msimu uliyopita

Real Madrid wameamua kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Ajax, Mholanzi Donny van de Beek, 22, badala ya kung’ang’ania usajili wa Mfaransa Paul Pogba, 26 kutoka Manchester United. (Marca)

Leicester inatathmini uwezekano wa kumsajili James Tarkowski, 26, wa Burnley ama Nathan Ake, 24, wa Bournemouth katika safu yao ya ulinzi kuchukua nafasi ya beki wao Muingereza Harry Maguire, 26, ambaye anahusishwa na harakati za kuhamia Man United. (Sky Sports)

Harry Maguire

Mabingwa Manchester City wanajiandaa kukamilisha usajili wa £32m wa beki wa Ureno Joao Cancelo, 25, huku beki wa pembeni Mbrazil Danilo, 28, akitarajiwa kuondoka. (Mail)

Tottenham wanapigiwa upatu kumjumuisha Josh Onomah, 22, katika mkataba wao wa £30m kumsaini mlinzi wa Fulham Ryan Sessegnon, 19. (Mail)

Crystal Palace wanajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania mwenye miaka 25- Victor Camarasa – ambaye msimu uliopita alikuwa Cardiff kwa mkopo. (Independent)Victor Camarasa akizungumza na kocha wa Cardiff Neil Warnock

Victor Camarasa akizungumza na kocha wa Cardiff Neil Warnock

Watford wamekataa dau la £32m kutoka kwa Everton kumnunua kiungo wa kati wa miaka 26 Mfaransa Abdoulaye Doucoure. (RMC, via Express)

Mshambuliaji wa Brentford, Mfaransa Neal Maupay 22, anatarajiwa kujiunga na Brighton kwa kandarasi ya miaka minne. (L’Equipe – in French)

Brighton inatarajiwa kukamilisha usajili wa Maupay kwa fedha za juu katika rekodi ya klabu hiyo. (Talksport)Wayne Rooney

Wayne Rooney

Nahodha wa zamani wa England Wayne Rooney, 33, anataka kurejea Manchester United kama kocha pale atakapostaafu kandanda. (Sun)

Rais wa Becelon Barcelona Josep Maria Bartomeu amegusia kuwa mabingwa hao wa Uhispania huenda watafanya usajili mwingine baada ya kuthibitisha kuwasili kwa Junior Firpo, 22, kutoka Real Betis. (Sport)

Inter Milan imemwambia mshambuliaji wa Argentina, Mauro Icardi, 26, kuwa hatacheza kwa miaka miwili ikiwa ataendelea kusisitiza kusalia katika klabu hiyo hadi mkataba wake utakapokamilika. (Gazzetta Dello Sport)Mauro Icardi

Mauro Icardi

West Ham wanapania kumsajili mchezaji wa tano kabla ya dirisha la usajili kufungwa lakini hawana mpango wa kumsaini mlinzi wa zamani wa Chelsea na kiungo wa kimataifa wa England Gary Cahill, 33. (Football.London)

Tetesi Bora Jumapili

Manchester United wamewasilisha ombi la dau la £46m kumsajili mchezaji wa Ajax mwenye umri wa miaka 22 na raia wa Brazil David Neres. (Yahoo – in Portuguese)

Arsenal wanatarajiwa kuanzisha mazungumzo na Barcelona kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Phillipe Coutinho 27 hatua ambayo itaigharimu klabu hiyo dau la £27m. (Sun on Sunday)Philippe Coutinho

Bayern Munich wanakaribia kumsajili winga wa Manchester City raia wa Ujerumani Leroy Sane baada ya kukubali kandarasi na masharti na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Sky Sport Germany – in German)

Mchezaji wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba anahofia huenda akashindwa kuelekea Real Madrid huku mabingwa hao wa Uhispania wakikabiliwa na dau la £270m kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Manchester United. (Sunday Mirror)

Paul Pogba

Pogba Pogba

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents