Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu hii Barcelona yajipanga kumpa mkataba mpya Lionel Messi, Pogba wengine sokoni

Barcelona wanaandaa mkataba mpya wa mshambuliaji Lionel Messi, 32, ambao utambakisha nyota huyo Camp Nou kwa miaka iliyosalia ya maisha yake ya soka. (Mundo Deportivo via Mirror)

Barcelona wanajiandaa kusaini mkataba na mshambuliaji wa mbele Lionel Messi, 32

Chelsea inaweza kulazimika kumpa mkataba wa muda mrefu beki wake wa kushoto Mbrazil Emerson Palmieri, mwenye umri wa miaka 25, ambaye kocha Maurizo Sarri anamyemelea kumpeleka Juventus. (Express)

Manchester United na Manchester City wapo mbioni kupambana kumsajili kiungo wa wa Benfica Florentino Luis mwenye umri wa miaka 20. (Star)Paul Pogba

Paul Pogba

Kiungo nyota wa Ufaransa Paul Pogba, 27, aliamua kusalia Manchester United badala ya kuhamia Real Madrid kutokana na mkataba wa pauni pauni 150 wa udhamini wa michezo . (The Sun)

Beki wa timu ya taifa ya Uholanzi Virgil van Dijk, 28, ameshangazwa na maneno kuwa atapewa ofa ya mpya ya mkataba wa malipo ya pauni na 200,000 kwa wiki na klabu yake ya Liverpool. (Liverpool Echo)

Kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 24, anakaribia kusaini mkataba mpya licha ya Manchester United kumtaka Mserbia huyo pamoja na vilabu vya Paris St-Germain na Juventus. (Daily Mail)Mchezaji wa safu ya ulinzi ya Uholanzi Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 28

Mchezaji wa safu ya ulinzi ya Uholanzi Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 28

Meneja wa zamani wa Leicester Mfaransa Claude Puel ndiye mtu anayetazamiwa kuchukua nafasi ya meneja katika klabu ya Ureno ya Sporting Lisbon.(L’Equipe)

Marcos Rojo, 29, atalazimisha kuhamia Aston Villa kutoka Manchester United mwezi Januari , baada ya mlinzi huyo wa Argentina kushindwa kuondoka Old Trafford katika dirisha la usajili lililoisha hivi karibuni. (Birmingham Live)

Kelechi Nwakali, 21, ambaye alihamia katika klabu ya daraja la pili ya Uhispania, Huesca kutoka Arsenal msimu huu , anataka kurudi katika uwanja wa Emirates siku zijazo . (Score Nigeria via Football.London)

Beki wa England Danny Rose, 29, anataka kuendela kupigania nafasi yake katika timu ya Tottenham Hotspur licha ya kwamba klabu nyingine zimeonyesha kumtaka na kuwasili kwa Ryan Sessegnon, mweny umri wa miaka 19, kutoka Fulham. (Mirror)Marcos Rojo, mwenye umri wa miaka 29, atalazimika kuhamia Aston Villa kutoka Manchester United mwezi Januari

Marcos Rojo, mwenye umri wa miaka 29, atalazimika kuhamia Aston Villa kutoka Manchester United mwezi Januari

Real Madrid watagrejelea tena haja yao ya kumsaka kiungo wa kati wa Ajax – Donny van de Beek,mwenye umri wa miaka 22, katika kipindi cha msimu kuhama kwa wachezaji cha majira ya kiangazi cha mwaka 2020 . (Daily Mail)

Leeds wanakaribia kabisa kuongeza zaidi mkataba wa miaka mitano na kiungo wa kati wa Kalvin Phillps mwenye umri wa miaka 23 ,baada ya Aston Villa na Burnle kuonyesha nia za kumnunua mchezaji huyo katika kipindi cha mechi za kipindi cha kabla ya kuaza kwa msimu wa michezo . (Telegraph)

Mchezaji wa safu ya nyuma wa Italy ukipenda full-back -Matteo Darmian, mwenye umri wa miaka 29, anasema hajutii kitendo chake cha kuhamia Manchester United,paada ya kujiunga na Parma kuhfuatia misimu minne akiwa katika Old Trafford. (Football Italia)

Mlinda lango wa Stalwart Germany na Bayern Munich Manuel Neuer, mwenye umri wa miaka 33, hana mipango ya kustaafu . (Mirror)

Waziri mkuu wa Albania Edvin Rama amefichua kuwa mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron aliomba msamaha wa dhati baada ya kupigwa kwa wimbo wa taifa ambao sio wa Albania kwa ajili ya timu ya nchi yake katika mchezo wa timu zilizofuzu kwa ajili ya kombe la Euro 2020 wakati wapocheza na timu ya Ufaransa mjini Paris. (Goal.com)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents