Soka saa 24!

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu hii Hazard, Coutinho, Pogba, Rice, Lacazette sokoni

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 28, anasema kuwa amaifahamisha klabu hiyo kuhusu amuzi wake wa kuhamia Real Madrid. (Daily Mail)

Eden Hazard

Blues pia wanataka kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 26, ikiwa rufaa waliowasilisha kwa shirikisho la FIFA dhidi kupinga marufuku ya usajili wa wachezaji itapita msimu huu. (Cadena Ser via Daily Mail)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amefutilia mbali mkutano wa mwisho wa msimu kwasababu alikuwa amekasirika baada ya timu yake kufungwa mabao 2-0 na Cardiff siku ya Jumapili. (The Sun)Ole Gunnar Solskjaer

Kiungo wa kati United Paul Pogba, 26, alirushiana maneno na mashabiki baada ya wao kusema kuwa anastahili kuuzwa baada ya kushindwa na Cardiff. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 27, anasema kuwa alishangazwa na tetesi zinazodai kuwa atahamia Barcelona. (Goal)Alexandre Lacazette

Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini amekiri kuwa huenda akamkosa kiungo wakati wa England Declan Rice, 20, ikiwa timu kubwa zitaonesha nia ya kumnunua. (Mirror)

Meneja wa Everton Marco Silva anasema kuwa hana uhakika ikiwa klabu hiyo itashinda kinyan’ganyiro cha kumsajili kwa mkopo kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes, 25, msimu ujao. (Liverpool Echo)

Kocha wa klabu ya Newcastle Rafael Benitez, 59, atafanya mkutano wa dharura na mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley wiki ijayo ili kujadili hatma yake ya baadae. (Daily Mail)Meneja wa Everton Marco Silva

Tetesi Bora Jumapili

Mesut Ozil, 30, hataondoka Arsenal msimu huu wa joto. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani atasalia Gunners hadi mkataba wake utakapokamilika.(Mirror)

Pep Guadiola amewahakikishia Manchester City kuwa hana mpango wa wa kuacha kazi katika klabu hiyo kwa miaka miwili licha ya tetesi kuwa huenda akajiunga na Juventus msimu huu wa joto.(Express)Josep Guardiola applauds

Manchester United wanamtaka kiungo wa kati wa Everton Idrissa Gueye,29. Everton inata karibu paunimilioni 40 kumuuza kiungo huyo wa kimataifa wa Senegal. (Mail)

Everton wameanzisha mazungumzo na Barcelona kuhusu uhamisho wa kudumu wa wa kungo wa kati wa Ureno Andre Gomes,25, anayechezea klabu hiyo kwa mkopo(LiverpoolEcho)

Andre Gomes

Buyern Munich bado wanamtaka winga wa Chelsea na kiungo wa kimataifa wa England Callum Hudson-Odoi,18 (Build- kwa Kijerumani)

Kumekua na mvutano mkubwa kati ya mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale na meneja Zinadine Zidane, kumaanisha kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Wales hana maisha katika klabu hiyo.(AS-in Spanish)

Tetesi Bora Jumamosi

Mshambuliaji wa Chelsea Ubelgiji Eden Hazard, 28, yuko katika harakati ya kukubali masharti mapya na Real Madrid kuhusiana na uhamisho mwisho wa msimu huu . (Independent)

Manchester United ilikosa fursa muhimu ya kumsaini nahodha wa klabu ya Ajax na uholanzi Matthijs de Ligt, 19, kwa kuwa iliambiwa kwamba mchezaji huyo atakjuwa mnene kupitia kiasi. (Mirror)Matthijs de Ligt

Winga wa Uingereza Jadon Sancho, 19, atasalia katika klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund mwisho wa msimu huu na kupinga kurudi katika ligi ya Uingereza. (Sun)

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW