Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu hii, Maguire kuwa beki ghali zaidi dunia, Liver na United zapigana vikumbo kwa kinda wa Real Betis, Firpo

Mchezaji wa Leicester City na Uingereza Harry Maguire, 26, anatarajiwa kuwa beki ghali zaidi duniani wiki hii wakati atakapojiunga na Manchester City kwa dau la £80m baada ya kukataa kujiunga na Manchester United. (Mirror)

Harry Maguire kuwa beki ghali zaidi duniani

Liverpool na Manchester United watapigania saini ya mchezaji wa Uhispania na Real Betis beki wa kushoto Junior Firpo, 22. (Marca)

Manchester United watatumia kifungo cha sheria ya kumuongezea miezi 12 Marcus Rashford katika kandarasi yake uku kukiwa na hofu kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 huenda akaondoka man United wakati mkataba wake utakapokamilika mwisho wa msimu ujao. (Sun)

Macus Rashford anataka kuondoka Man United
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Inter Milan haijaafikia kiwango cha £22.3m kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Ubelgiji Romelu Lukaku, 26. (La Gazzetta dello Sport, via Football Italia)

Romelu Lukaku

Newcastle United inatarajiwa kufanya majaribio ya mwisho kumrai mkufunzi Rafael Benitez kuongeza kandarasi yake.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 , ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa mwezi Juni ameripotiwa kupata kazi nchini China. (Evening Chronicle)

Divock Origi

Real Betis wana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Ubelgiji Divock Origi, 24. (Estadio Deportivo, in Spanish)

Klabu ya Brighton imekubali kumsajili winga wa Ubelgiji Leandro Trossard, 24, kutoka Genk kwa dau la £18m. (Sky Sports)

Mchezaji anayelengwa na Liverpool Nicolas Pepe anawaniwa na InterMilan kwa dau la £80m.

Nicolas PepHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Timu hiyo ya Ligi ya Serie A Inter Milan ni miongoni mwa klabu nyingi zilizo na hamu ya kumsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Lille na Ivory Coast . (L’Equipe, in French)

Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer amewasilisha ombi la kibinafsi kwa afisa mkuu mtendaji -mwenyekiti Ed Woodward kuharakisha ili kumsajili kiungo wa kati wa Lisbon na Portugal Bruno Fernandes , 24, (Record, in Portuguese, subscription required)

Lucas Torreira

Wakati huohuo Manchester United wako katika harakati za kumsaini winga wa Uhispania mwenye umri wa miaka 16 Mateo Mejia kwa dau la £600,000 kutoka klabu ya Real Zaragoza. (Sun)

Arsenal inafikiria kumuuza Lucas Torriera, 23, baada ya AC Milan kuwasilisha ombi lao la kwanza kwa kiungo huyo wa Uruguay. (Sport Mediaset, in Italian)

Mkufunzi wa Leicester Brendan Rodgers ameambiwa kwamba anapoteza wakati kujaribu kumsaini kiungo wa kati wa Uskochi mwenye umri wa miaka 26 Callum McGregor kutoka klabu yake ya zamani Celtic. (Scottish Daily Mail)

AZ Alkmaar imethibitisha mazungumzo na kiungo wa kati wa Southampton Jordy Clasie, 27. (Daily Echo)

Klabu ya Uholanzi ya AZ Alkmaar imethibitisha mazungumzo na kiungo wa kati wa Southampton Jordy Clasie, 27. (Daily Echo)

Burnley wamemwambia beki Ben Gibson,26, anaweza kuondoka mwisho wa msimu huu.

Anston Villa ambao wamepanda daraja la ligi ya Premier pamoja na Sheffield United ni miongoni mwa kundi la klabu zilizo na hamu ya kumsaini mchezaji huyo wa Uingereza kwa dau la £15m. (Teamtalk)

Aston Villa wanatarajiwa kuanza mazungumzo ya kumsajili beki wa Bournemouth Tyrone Mings,26. Mchezaji huyo wa Uingereza alikuwa kiungo muhimu katika kupandishwa daraja kwa Villa wakati alipoichezea klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita.. (Birmingham Mail)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents