Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu hii, Pogba, Eden Hazard, Joe Hart

Wachezaji wa Manchester United wanataniana ‘hadharani” kuhusu tetesi za uhamisho wa Paul Pogba kwenda Real Madrid.

Martial na Pogba

Pogba, 26, ameonekana akiwatania wenzake kuwa anataka kujiunga na Real Madrid. (AS – in Spanish)

Mchezaji nyota wa Chelsea Eden Hazard amepigwa picha akiwa amevalia jezi mpya ya mazoezi ya klabu hiyo.

Hatua hiyo imewapa matumaini mashabiki wa Blues kwamba Hazard ambaye pia ni kiungo kimataifa wa Ubelgiji atasalia Stamford Bridge msimu ujao. (Express)

Ubelgiji inamfuatilia Thorgan Hazard, ambaye ni ndugu ya Eden, na inasema kuwa kiungo huyo wa miaka 26 amekubali kujiunga na Borussia Dortmund na kwamba anasubiri klabu yake ya sasa Borussia Monchengladbach kuidhinisha uhamisho wake. (VTM Nieuws – in Dutch)

Kipa Joe Hart, 32, yuko huru kuondoka Burnley kwa uhamisho bila malipo msimu huu wa joto, huku vilabu kadhaa vya Ligue 1 vikionesha azma ya kutaka kumsajili. (Mail)

Joe Hart

Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers amesema kuwa klabu hiyo itafanya kila iwezalo kuhakikisha inampampatia mkataba wa kudumu kiungo wa kati wa Monako Youri Tieleman, 21, msimu ujao. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Foxe James Maddison ametoa wito kwa klabu yake kumsaini kiungo huyo wa kimataifa wa Ubegiji. (Leicester Mercury)

Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Gennaro Gattuso katika klabu ya AC Milan. (Evening Standard)

Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri

Manchester United imeungana na Liverpool katika kinyang’anyiro cha kusaini mshambuliaji wa Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe, 23 ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa paini milioni 60. (Express)

Kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic, 31, amesema kuwa atasalia Barcelona hadi mkataba wake wa sasa utakapokamilika mwaka 2021. (Marca)

Nicolas Otamendi ataondoka Manchester City msimu huu, na tayari West Ham na Wolves wanataka kumsaini mlinzi huyo wamiaka 31. (Star)

Nicolas Otamendi

Mpango wa Chelsea msimu ujao ni huenda ukaathiriwa na marufuku ya usajili wa wachezaji Fifa dhidi yao. (Evening Standard)

Bournemouth wanapania kumsajili beki wa nyuma na kati wa West Brom Dara O’Shea, 20, amabaye amekuwa akichezea klabu ya daraja la pili Exeter City. (Mail)

Kipa wa Barcelona na Uholanzi Jasper Cillessen, 30, amesema kuwa anataka kuondoka Nou Camp msimu huu baada ya kushindwa kumuondo Marc-Andre ter Stegen. (Ziggo Sport, via Marca)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents