Burudani ya Michezo Live

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu hii, PSG kumsajili Dybala, Coutinho atua Bayern Munich na wengine sokoni 

Mabingwa wa Ufaransa PSG wamefanya mazungumzo na Juventus kuhusu uhamisho wa dau la pauni milioni 73 kumsajili mshambuliaji wa Argentina mwenye umri wa miaka 25 Paulo Dybala. (Mail)

Paulo Dubala

Kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho amewasili nchini Ujerumani ili kukamilisha mkopo wake wa msimu huu kwa mabingwa wa ujerumani Bayern Munich. (Sun)

Image result for Philippe Coutinho has arrived in Germany

Paris St-Germain wamemtaka beki wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane, 26, pamoja na mshambuliaji wa Brazil Vinicius Junior, 19, katika mpango wa kubadilishana wachezaji iwapo wanamuitaji mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 Neymar. (Telefoot – in French)

Varane

Barcelona inatumai kumrudisha Neymar Nou Camp , lakini kukiwa na kifungu cha kumnunua.. (Sport – in Spanish)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Tottenham Fernando Llorente, 34, anakaribia kujiunga na klabu ya Itali Lazio. Inter Milan, Fiorentina na Napoli pia zina hamu ya kumsaini raia huyo wa Uhispania , ambaye kwa sasa hana klabu. (Corriere Dello Sport – in Italian)

Inter Milan wanataka kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Chile Alexis Sanchez, 30, na pia wana hamu na mshambuliaji Llorente na kiungo wa kati wa Barcelona na raia wa Chile Arturo Vidal, 32. (Gazzetta dello Sport – in Italian)Alexi Sanchez

Ajenti wa Sanchez yuko nchini Uingereza kuzungumzia mkopo wake kuelekea Inter Milan. (Sky Italy, via Sky Sports)

Sanchez alikua akifanya mazoezi na United siku ya Jumapili alfajiri.. (The Sun)

Inter Milan inajaribu kuafikia makubaliano ya kumnunua Sanchez lakini United imelazimika kumtoa kwa mkopo ili kutolipa mshahara wake wa £500,000 kwa wiki. (Mirror)Eric Bailey

Manchester United wanatarajiwa kuanza mazungumzo ya kumuongezea kandarasi beki Eric Bailey mchezaji mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ivory Coast . (Sun)

Paris St-Germain na Bayern Munich huenda zikawasilisha ombi kumnunua kiungo wa kati wa Ujerumani Emre Can, 25, baada ya kuambiwa na mkufunzi wake Maurizio Sarri anahitajiki Juventus. (Tuttosport, via Mail)

Paris St-Germain na Monaco zinafikiria kumpatia ofa kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 25, kwa kuwa muda wake Chelsea unaonekana kwamba umekwisha.. (Daily Express)Tiemou Bakayoko

Celtic imeipatia ofa Bordeaux kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa Olivier Ntcham . (20 Minutes via Daily Record)

Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce yuko tayari kumrudisha uwanjani mshambuliaji wa England Dwight Gayle, 28, haraka iwezekanavyo. (Newcastle Chronicle)

TETESI ZA SOKA JUMAPILIJadon Sancho

Jadon Sancho anatarajiwa kuondoka Borussia Dortmund msimu ujao huku klabu hiyo ya Ujerumani ikimtafuta mchezaji atakayechukua mahala pake. (Mail)

Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema kwamba winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, huenda akaondoka katika klabu hiyo msimu huu . (Sun)

Mshambuliaji wa Manchester United na Chile Alexis Sanchez, 30, amekataa uhamisho wa kuelekea Roma, licha ya klabu hiyo ya Old Traford kukubali kulipa kitita kikubwa cha mshahara wake wa £560k kwa wiki.{Mirror)Sanchez

Hatahivyo Sanchez huenda akaelekea katika ligi ya serie A baada ya Man United kumruhusu kufanya mazungumzo na Inter Milan, ambapo huenda akakubali kupunguza mshahara wake. (Mail)

Liverpool huenda ikafaidika na £18m iwapo mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo na raia wa Brazil Philippe Coutinho, 27, ataelekea Bayern Munich kwa mkopo. (Mail)

Coutinho

Everton imetoa ofa ya kumsaini winga wa Ufaransa Franck Ribery, 36, ambaye yupo huru baada ya kuondoka Bayern Munich baada ya kuhudumu kwa miaka 12 katika klabu hiyo ambayo ndio mabingwa wa ligi ya Bundesliga . (90Min)

Kwengineko, kiungo wa kati wa Portugal Renato Sanches, 21, anataka kuondoka Bayern kwa kukosa muda wa kucheza katika klabu hiyo. (Sport1 – in German)Mesut Ozil

Mesut Ozil, 30, huenda akaondoka Arsenal na kujiunga na klabu ya DC United iwapo klabu hiyo ya ligi ya MLS inaweza kumshawishi kiungo huyo wa Ujerumani kuhamia Washington. (Star)

Beki wa kulia wa Ivory Coast Serge Aurier, 26, huenda akaondoka Tottenham na kuelekea AC Milan iwapo beki wa timu hiyo Andrea Conti, 25, ataondoka ligi ya Serie A kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho la Ulaya. (Calciomercato)

Na mchezaji wa Everton Yannick Bolasie, 30, yuko tayari kurudi katika uwanja wa Goodison Park, huku klabu za Uturuki Besiktas na Trabzonspor zikiwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa Congo . (Sun)Mchezaji yannick Bolassie wa Congo

Mchezaji wa zamani wa Manchester City na Liverpool Mario Balotelli, 29, anakaribia kujiunga na klabu ya Serie A Brescia. (Sun via La Gazzetta)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 27, hakuorodheshwa katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya Rennes kutokana na jeraha na sio kwamba raia huyo wa Brazil anataka kurudi Barcelona. (AS – in Spanish)

Mshambuliaji wa Barcelona Kevin-Prince Boateng, 32, amefichua ni kwa nini Sir Alex Ferguson hakumsajili kujiunga na Manchester United mapema wakati wa kipindi chake cha mchezo. (Goal)Neymar

Mchezaji mpya wa Man United Hannibal Mejbri, ambaye aliwasili kutoka Monaco na hawezi kutia kandarasi ya mchezaji wa kulipwa hadi atakapofikisha umri wa miaka 17 January, anataka kuvaa jezi nambari saba Old Trafford. (Mirror)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW