Tupo Nawe

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu hii, Zidane, Mourinho, Martial, Valencia, Christensen, Adams

Aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane atakubali kuifunza Chelsea na kuchukua mahala pake Maurizio Sarri iwapo atapewa £200m kutumia huku klabu hiyo ikimpatia mshambuliaji wake Eden Hazard kandarasi mpya. (Sun)

Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 23, na mshambuliaji wa Uingereza Jesse Lingard, 26, huenda wakarudi katika ,mechi dhidi ya Liverpool Jumapili ijayo , licha ya kudaiwa kwamba huenda wakakosa kati ya wiki mbili au tatu na mkufunzi wao Ole Gunnar Solskjaer. (Mirror)

West Ham inajiandaa kuwasilisha ombi la kumnunua winga wa Ecuador na Manchester United Antonio Valencia, 33, iwapo beki wa kulia wa Argentina Pablo Zabaleta, 34, ataamua kustaafu mwisho wa msimu huu. (Mail)

Beki wa Chelsea na Denmark Andreas Christensen, 22, amekana kwamba anataka kuondoka katika klabu ya Stamford bridge , baada ya kuona muda wake wa kushiriki katika mechi umepunguzwa chini ya Maurizo Sarri . (Bold via Football London)

Mshambulaiji wa Brazil Neymar, 27, hajaamua kuondoka katika klabu ya Paris St-Germain kulingana na babake ambaye aliongezea kuwa soka inaweza kubadilika wakati wowote.. (Le Perisien – In French)

Manchester United na Arsenal hawana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Birmingham City na Uingereza Che Adams, 22. (Mirror)

Arsenal inajiandaa kumnunua kipa wa Burnley na Uingereza Nick Pope, 26, ambaye ameshindwa kuchukua nafasi yake ya kwanza katika uwanja wa Turf Moor baada ya kupata jeraha. (Sun)

Mesut Ozil

Pia kiungo wa kati wa klabu ya Arsenal na Ujerumani Mezut Ozil, 30, ameondoka mjini London na kuhamia Uturuki kwa siku chache baada ya kuwachwa nje katika kikosi cha Arsenal cha kombe la Yuropa katikati ya wiki hii. (Mirror)

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United, Chelsea na Real Madrid Jose Mourinho huenda akaifunza klabu ya daraja la kwanza nchini Ufaransa. (Bein Sports)

Jose Mourinho

Ufunguzi wa uwanja mpya wa klabu ya Tottenham umecheleweshwa hadi mwezi Aprili kutokana na mipangilio ya mechi za kombe la FA Cup . (Sun)

Manchester United iko tayari kuilipa Tottenham fidia ya £34m ili kumsajili mkufunzi wake Mauricio Pochettino kama mkufunzi wao wa kudumu mwisho wa msimu huu.(Standard)

Mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 29, sio maarufu miongoni mwa wachezaji wenzake katika uwanja wa Bernabeu, na anajulikana kama ‘The Golfer’, kulingana na kipa wa klabu hiyo Thibaut Courtois. (Mail)Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW