Aisee DSTV!

Tetesi za soka barani Ulaya, Man United wamkomalia Bruno Fernandes, Maguire apewa ruhusa ya kuondoka Leicester

Tetesi za soka barani Ulaya, Barcelona na njaa ya usajili waliwinda jembe hili, Man United wamkomalia Bruno Fernandes, habari ya Pogba zaanza kufifia

Kiungo wa Real Madrid, Dani Ceballos,22, karibuni kujiunga na Arsenal. (Mundo Deportivo). Kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen,27, ni moja ya majina yaliyowekwa wazi na Atletico wakiwa wanatazamia kumsajili mchezaji huyo. (Evening Standard)

Mlinzi wa kushoto wa timu ya taifa ya England Danny Rose, 29, hatasafiri na Spurs kwenda Singapore, huku ikielezwa kuwa yuko sokoni. (Telegraph)

Manchester United imetoa ofa ya donge nono kumnyakua kiungo Bruno Fernandes, 24, wa Sporting Lisbon. (Mirror)

Barcelona wana mpango wa kumsajili beki wa kushoto Junior Firpo, 22, wa Real Betis kuziba nafasi ya Jordi Alba. (Marca)

Kiungo wa kati wa Tottenham na timu ya taifa ya Denmark Christian EriksenHaki miliki ya pichaREUTERS

William Saliba anataka kuhamia Arsenal lakini timu yake , St Etienne imevutiwa na ofa ya tottenham kwa mchezaji huyo wa miaka 28. (the sun)

Cardiff City imepiga hatua muhimu ya kutaka kufanya mazungumzo na klabu ya Bordeaux ya ufaransa kuhusu mchezaji Younousse Sankhare,29, baada ya kuachwa kwa kiungo huyo na timu yake katika mechi za maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani. (Wales Online)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi ya Atalanta Gianluca Mancini anajiandaa kuhamia Roma kwa kitita cha pauni milioni 26. (Gazzetta dello Sport )

Mchezaji wa timu ya St. Etienne, William SalibaHaki miliki ya pichaREUTERS

Parma imemsajili tena mshambuliaji Roberto Inglese, 27, kutoka Napoli kwa mkopo- ingawa klabu hiyo inawajibika kumnunua. (Corriere dello Sport – in Italian)

Liverpool imemjumuisha Andy Linergan, 35, kwenye mechi za maandalizi, Amerika Kaskazini kuziba nafasi ya mlinda mlango. . (Daily Mail)

Leicester imemwambia mlinzi wake wa kati Harry Maguire, 26, kuwa anaweza kuondoka (Telegraph)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 27, amerejelea kauli yake uhusu nia yake ya kuondoka kwenye klabu hiyo kwenye mkutano wake na mkurugenzi wa ufundi Leonardo . (ESPN)

Newcastle watalipa pauni milioni 4 kama fidia kwa timu ya Sheffield Wednesday kwa ajili ya kocha wao wa zamani Steve Bruce.(Sun)

Wasaidizi wa Bruce Steve Agnew na Stephen Clemence pia wameondoka Sheffield Wednesday na watajiunga naye St James’Park .(Newcastle Chronicle)

Manchester United watapeleka rasmi ofa ya kumnasa kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 24, katika kipindi cha majuma matatu yajayo.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW