Aisee DSTV!

Tetesi za soka barani Ulaya, pauni milioni 100 za usajili za mpa ukichaa Ole Gunnar, Pogba sokoni Neymar kutua Madrid kubadilishwa na Bale au James na wengine sokoni

Tetesi za soka barani Ulaya, pauni milioni 100 za usajili za mpa ukichaa Ole Gunnar, Pogba sokoni Neymar kutua Madrid kubadilishwa na Bale au James na wengine sokoni

Juhudi za kocha Ole Gunnar Solskjaer kuimarisha kikosi chake huenda zikagonga mwamba kwa sababu Manchester United ni klabu ambayo hutoa ofa ya chini kwa wachezaji wanaotaka kuwasajili. (Evening Standard)

Solskjaer anataka kumuuza kiungo wa kati wa Man Utd Mfaransa Paul Pogba, 26, bada ya kufahamishwa kuwa ana pauni milioni 100 ya kuwasajili wachezaji wapya msimu huu. (Star)

Mchezaji nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27, hana mpango wa kuchezea tena Paris St-Germain. (Sport – in Spanish)

Real Madrid wameweka dau la euro milioni 130 kumnunua Neymar, kutoka PSG, mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, au mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, 27. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Neymar katika mazoeziHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Atletico Madrid wanakaribia kukamilisha usajili wa Joao Felix wa Benfica kwa kima cha euro milioni 120 sawa na (£106.7m) hii ina maanisha Manchester United watamkosa kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno aliye na umri wa miaka 19. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Mhispania Rodri, ameamua kujiunga na Man City badala ya Bayern Munich na kuhamia City kawa malipo ua £62m. (Kicker – in German)

Manchester City wanapigiwa upatu kuipiku Man Utd katika usajili wa Harry Maguire, 26, kutoka Leicester kwa kima cha pauni milioni 65 baada ya kiungo huyo wa England kupita vipimo vya matibabu. (Star)

Harry MaguireHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Man City wanatafakari uwezekano wa kumsaini kwa mkataba wa bure Asier Riesgo wa ibar na kumfanya Mhispania huyo wa miaka 35 kuwa kipa wao wa tatu. (Manchester Evening News)

Everton wameanza maungumzo na Chelsea kuhusu usajili wa Kurt Zouma kwa mkataba wa kudumu baada ya mlinzi huyo wa Ufaransa, 24, kucheza Goodison Park msimu uliopita kwa mkopo katika. (Telegraph)

Tottenham wamefanya mazungumzo na ajenti wa kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24, kuhusu uhamisho wake kutoka Sporting Lisbon. (Telegraph)

Bruno FernandesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBruno Fernandes

Juventus wanamatumaini ya kufukia mkataba wa kumsaini Adrien Rabiot kutoka Paris St-Germain, huku mkataba wa mchezaji huyo raia wa Ufaransa anaechezea safu ya kati ukitarajiwa kukamilika msimu huu wa joto. (Goal)

Liverpool hawana mpango wa kumuuza Divock Origi msimu huu wa joto licha ya mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mweye umri wa miaka 24 kusalia na mkataba wa mwaka mmoja. (Liverpool Echo)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW