Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya, Sanchez agoma kuondoka Man United, Solskjaer amuambia atasugua benchi wengine sokoni 

Alexis Sanchez anakataa kuondoka Manchester United msimu huu, pamoja na kwamba kocha Ole Gunnar Solskjaer kutishia kumfanya kuwa mchezaji wa akiba ikiwa atasalia na timu hiyo. Roma inatafuta wachezaji wengine. (Sun)

Mchezaji wa Manchester United Alexis Sanchez

Hatahivyo, timu ya Serie A, AC Milan, Juventus na Napoli bado wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Chile, 30. (Mail)

Real Madrid imekataa ombi la Paris St-Germain kumjumuisha Vinicius Junior,19, katika ofa ya kumnyakua mshambuliaji wa Brazil Neymar,27. (AS)

Mbali na Vinicius, PSG wanapendelea Real wamjumuishe kiungo wa croatia Luka Modric,33 na kiungo wa Brazil Casemiro,27, kumpata Neymar. (Marca)

Neymar alikuwa mazoezini mwenyewe siku ya Jumatano, ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapouzwa.(Esporte Interactivo, via Mundo Deportivo – in Spanish)NeymarHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Kiungo mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 27, anaweza bado kujiunga na PSG ikiwa hatakuwa sehemu ya ofa ya Neymar. (Goal)

Beki wa kati wa Manchester United Victor Lindelof, 25, anajiandaa kusaini mkataba mpya kwa ongezeko la mshahara mbali na pauni 75,000 alizokuwa akipata kwa wiki. (Aftonbladet – in Swedish)

Bayern Munich huenda wakafufua nia yao ya kumnasa winga wa Manchester City, Leroy Sane, ingawa mchezaji huyo, 23, ana jeraha la mguu, litakalo mfanya kuwa nje ya uwanja kwa miezi saba. (Bild – in German)

Mshambuliaji wa Marseille na Italia Mario Balotelli,29, anajiandaa kutia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Brescia baada ya kukataa ofa ya Flamengo ya Brazil. (Guardian)

Flamengo bado wana matumaini ya kubadili msimamo wa Balotelli, baada ya kukubali ombi lake la kumsajili kaka yake Enock kucheza katika moja kati ya timu zao nyingine (Gazzetta dello Sport – in Italian)

Mshambuliaji wa Marseille na Italia Mario BalotelliHaki miliki ya pichaREUTERS

Winga wa klabu ya Everton Alex Iwobi, 23, amesema aliondoka Arsenal katika siku ya mwisho ya usajili kuthibitisha kuwa yeye si mchezaji anayechipukia tena. (Mirror)

Tottenham itazungumza na Christian Eriksen, 27,tena kuhusu mkataba mpya kabla kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, tarehe 2 mwezi Septemba, baada ya Real Madrid na Juventus kuonesha nia ya kumnasa kiungo huyo.(Independent)

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge, anaonekana kujiandaa kujiunga na timu ya Trabzonspor ya Uturuki kwa dili la pauni milioni 2.8 kwa kila msimu.(Goal)

Monaco imeingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwasajili wachezaji kiungo Blaise Matuidi,32, na beki wa kati Daniele Rugani,25, kutoka Juventus. (Gazzetta dello Sport – in Italian)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents