Uncategorized

Tetesi za soka Jumamosi hii Zaha, Lukaku, Pogba, De Gea, Sane, Jesus, Danilo, Tagliafico

Mchezaji wa safu ya mashambulizi Ivory ya Coast Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 26,amesema yuko tayari kuondoka Crystal Palace na anataka kucheza Championi Ligi. (Mail)

Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 26,amesema yuko tayari kuondoka Crystal Palace na anataka kucheza Championi Ligi

Manchester United wanajiandaa kusikia ni nini Romelu Lukaku atakachotaka msimu huu, huku mshambuliaji huyo mwenye mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ubelgiji akiwa tayari kuondoka Old Trafford. (Telegraph)

Mshambuliaji wa safu ya kati Mfaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, na mlinda lango Muhispania David de Gea,mwenye umri wa miaka 28,wametumia hali ya sintofahamu juu ya ikiwa Manchester watafuzu kwa ajili ya Championi Ligi au la kudai ongezeko kubwa la mshahara ili wabaki Old Trafford. (Times – subscription required)

David de Gea na Pogba wanasemekana kutumia sintofahamu juu ya ikiwa Manchester United watafuzu kwa Chambpioni Ligi kw akudai malipo ya juu zaidi

Kiungo wa kati Mjerumani Leroy Sane,mwenye umri wa miaka 23, na mshambuliaji kutoka Brazil Gabriel Jesus, mwenye umri wa miaka 22, ni wachezaji wawili tu miongoni mwa wachezaji takribani wanane walioombwa kuondoka Manchester City ikatika msimu ujao. (El Chiringuito, via Sun)

Inter Milan wanafanya mashauriano na mchezaji wa kimataifa wa safu ya ulinzi ya Manchester City Mbrazilo Danilo, mwenye umri wa miaka 27. (Calciomercato)

Mchezaji wa Arsenal Nicolas Tagliafico, mwenye umri wa miaka 26, amekataa ofa ya mkataba mpya na Ajax na muwakilishi wake, Ricardo Schlieper, amedokeza kuwa mlinzi huyo wa Argentina angependelea kuhamia Italia. (Football London)

Real Madrid bado ina matumaini ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Paris St-Germain Mbrazili Neymar,ambaye ana umri wa miaka 27 kwa sasa. (Marca)Wasichana wawili wakamatwa kwa ‘kupanga mauaji tisa’

Timu hiyo inayoongoza katika Ligi ya Uhispania pia wanakamilisha mkataba wa kumchukua mshambuliaji Mserbia Luka Jovic, mwenye umri wa miaka 21 kutoka Eintracht Frankfurt . (Star)

Real Madrid bado ina matumaini ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Paris St-Germain Mbrazili Neymar

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri ameonyesha dalilli kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Mfaransa Olivier Giroud mwenye umri wa miaka 32 hataondoka Chelsea msimu ujao (Telegraph)

Napoli wanaangalia uwezekano wa kumchukua mchezaji wa safu ya nyuma wa Tottenham na England Kieran Trippier, mwenye umri wa miaka 28. (Football Italia)

Arsenal na Everton wanaangalia uwezekano kumuhamisha mshambuliaji Fortuna Dusseldorf ya Mbelgiji Benito Raman,mwenye umri wa miaka 24 kwa £13m . (Bild, via Sun)

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez kulipwa £50m kila mwaka , kabla ya mauzo ya mchezaji , kama atakubali kusaini mkataba mpya

Meneja wa Burnley Sean Dyche hawezi kusema mengi juu ya yale anayoyafikiria kuhusu thamani ya Dwight McNeil baada ya winga huyo wa Uingereza kwenye umri wa miaka 19- kusemekana anatakiwa na Arsenal, Manchester City, Liverpool, Everton na Newcastle. (Burnley Express)

Newcastle imemuambia meneja Rafael Benitez atakuwa anapewa £50m kila mwaka , kabla ya mauzo ya mchezaji , kama atakubali kusaini mkataba mpya . (Independent)

Mchezaji wa safu ya kati wa Southampton kutoka Northern Irish Steven Davis, mwenye umri wa miaka 34, anayecheza kwa deni katika Rangers, ameanza mazungumzo na klabu ya Uskochi juu ya kuhama msimu huu. (Sky Sports)

Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde amemuelezea Pep Guardiola kama mtu aliye bora zaidi katika biashara, licha ya Manchester City kuendolewa katika Championi Ligina Tottenham. (Marca)


Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents