Aisee DSTV!

Tetesi za usajii barani Ulaya, Real Madrid waandaa mkakati wa kumnasa Pogba, Unai Emery aeleza mikakati ya kuwanasa wachezaji kadhaa Arsenal

Real Madrid wana mpango wa kuanzisha ”operesheni 200” wakiwa na mpango wa kuwauza Gareth Bale, 30 na James Rodriguez, kwa ajili ya kuuwezesha kifedha mpango wao wa kumnunua kiungo Paul Pogba. (Marca, via Sun). Neymar amefungua milango kwa United wakati akiwa na shauku ya kuondoka Paris Saint-Germain. (Mundo Deportivo, via Sun)

Kocha mkuu wa Newcastle Steve Bruce kutumia zaidi ya pauni milioni 90 katika dirisha la usajili. (Sky Sports)

Bruce ‘alikuwa chaguo la 11’ kwa ajili ya kazi hiyo ndani ya Newcastle. (Daily Mail)

Hoffenheim wamethibitisha kuwa mshambuliaji Joelinton, 22, yuko kwenye ”mazungumzo ya kina” na klabu hiyo na Newcastle United wana matumaini ya kuvunja rekodi kumnasa mchezaji huyo mwenye asili ya Brazil. (Chronicle Live)

Kocha wa Leicester Brendan Rodgers amesifu utaalamu wa Harry Maguire, 26, na kukubali kuwa alikuwa ”ametulia” kuhusu nia ya Manchester United kumnasa mlinzi huyo wa kati .(Independent)

Liverpool haina mpango kabisa wa kumuuza golikipa Simon Mignolet, 31 kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Liverpool Echo)

Manchester United iko kwenye kinyang’anyiro cha kuwania saini ya kiungo wa Roma Nicolo Zaniolo. (Mirror)

Mshambulizi Romelu Lukaku, 26, ana mpango wa kuondoka Manchester United na kuhamia Inter Milan. (Times – subscription required)

Unai Emery amesisitiza kuwa Arsenal wanafanya kazi kupata wachezaji ”watatu au wanne kabla ya kuanza msimu mpya. (Independent)

Kiungo Granit Xhaka yuko kwenye nafasi ya kuwa nahodha wa Arsenal akichukua nafasi ya Koscielny. (Telegraph)

Wadau wa klabu ya Juventus wamempa wakala wa Matthijs de Ligt mapokezi makubwa wakati alipoambatana na mchezaji huyo, mwenye miaka 19 kwa ajili ya vipimo siku ya Jumatano. (Metro)

Mchezaji wa Crystal Palace Wilfried ZahaHaki miliki ya pichaREUTERS

Mchakato wa Arsenal kumpata mlinzi wa kikosi cha Celtic, raia wa Scotland Kieran Tierney huenda ukapata upinzani kumnasa mchezaji huyo. . (Scotsman)

Arsenal imepewa angalizo kuwa haitaweza kufikia dau la Crystal Palace kwa ajili ya mshambuliaji Wilfred Zaha. (Mirror)

Pep Guardiola amefungua milango kwa Leroy Sane, 23, kuondoka Manchester City kwa kumwambia winga huyo anaweza kufanya hivyo kama hana furaha. (Mirror)

Burnley wana nia ya kumuuza golikipa wa kimataifa Tom Heaton wa England, kwa pauni milioni 12. (Birmingham Mail)

Ashley Cole amesababisha minong’ono kuwa yuko mbioni kuingia kwenye jopo la makocha wa Chelsea, baada ya kuweka picha yake akiwa uwanja wa ndege akielekea Japan. (Mirror)

Chanzo BBC.
By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW