Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya alhamisi hii, De Gea, Varane, Schurrle, Niguez, Rodri, Walcott na wengine sokoni

Klabu ya Manchester United imesema hawatalazimishwa kumuuza mlinda mlango David de Gea, raia wa Uhispania mwenye umri wa miaka 28, mwishoni mwa msimu – hata kama watashindwa kukubaliana naye juu ya mkataba mpya , jambo linalochochea uwezekano wa kuwa huru kuondoka mwishoni mwa msimu ujao . (Mirror)

Real Madrid, Juventus na Paris St-Germain wote wanafuatilia kwa karibu hali ya De Gea . (Express)

Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anataka kusaini wachezaji wapya watano. (Telegraph)

Ander Herrera anaweza kuondoka Manchester United msimu huu
Image captionAnder Herrera anaweza kuondoka Manchester United msimu huu

Manchester United imejiunga katika mbio za kumsaka mchezaji wa safu ya kati wa Uhispania Saul Niguez, mwenye umri wa miaka 24, huku Manchester City ikimchagua identifying mchezaji mwenzake katika timu za Atletico Madrid na Uhispania anayecheza safu ya kati Rodri Hernandez, mwenye umri wa miaka 22-kama mchezaji mbadala wanayelenga kumchukua. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Uhispania Ander Herrera, akiwa na umri wa miaka 29, anaweza kuondoka Manchester United msimu huu baada ya kughadhabishwa na hali ya mkataba wake katika Manchester United. (Mail)

Paris St-Germain na Manchester United wanamtaka mlinzi wa Ufaransa anayechezea Real kwa sasa Raphael Varane(mbele)
Image captionParis St-Germain na Manchester United wanamtaka mlinzi wa Ufaransa anayechezea Real kwa sasa Raphael Varane(mbele)

Manchester United wanaamini wanawataka wachezaji wa England wa kimataifa – winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, akiwa na umri wa miaka 19, na winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, mwenye umri wa miaka 18 – watatakiwa kuamua kutoendelea kuchezea klabu zao ambazo zimeshikilia msimamo kuwa haziko tayari kuwauza . (Mail)

Everton wameambiwa wajiandae kwa kuhama kwa kiungo wao wa kati Msenegali Idrissa Gueye
Image captionEverton wameambiwa wajiandae kwa kuhama kwa kiungo wao wa kati Msenegali Idrissa Gueye

Paris St-Germain na Manchester United wametoa ombi la awali kwa mlinzi wa Ufaransa anayechezea Real kwa sasa Raphael Varane, 25. (independent)

Mchezaji wa safu ya mbele Mjerumani Andre Schurrle, mwenye umri wa miaka 28, atakua muathiriwa wa kwanza wa kushushwa daraja katika timu ya Fulham kwa kurudishwa Borussia Dortmund mwaka mmoja kabla ya muda wake. (Sun)

Wachezaji wa timu ya Barcelona, kwabu hiyo imesema inatarajia kupata kati ya euro milioni 250 na milioni 300 kwa mauzo ya wachezaji msimu huu.
Image captionBarcelona inatarajia kupata kati ya euro milioni 250 na milioni 300 kwa mauzo ya wachezaji msimu huu.

Everton wameambiwa wajiandae kwa kuhama kwa kiungo wao wa kati Msenegali Idrissa Gueye ambaye sasa ana umri wa miaka 29 msimu huu . (Liverpool Echo

Winga wa zamani wa England Theo Walcott, mwenye umri wa miaka 30, anaweza kuwa muathiriwa wa kwanza wa mpango mpya wa Everton wa kuwalenga vijana chipukizi katika soko la wachezaji wanaohama. (Mirror)

Barcelona inatarajia kupata kati ya euro milioni 250 na milioni 300 kwa mauzo ya wachezaji msimu huu ili kuongeza fedha kwenye akaunti za klabu na hivyo kuwa na uwezo wa kusaini mikata mipya bila kujihatarisha kifedha. (ESPN)

Marc Overmars ni miongoni mwa watahiniwa wa kazi ya meneja wa masuala ya kiufundi wa klabu ya Arsenal
Image captionMarc Overmars ni miongoni mwa watahiniwa wa kazi ya meneja wa masuala ya kiufundi wa klabu ya Arsenal

Kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic, mwenye umri wa miaka 24, angependa abakie Chelsea, ambako anacheza kwa mkopo kuliko kurudi kwa klabu mama Real Madrid msimu ujao. (Goal)

Arsenal wamekuwa wakiwafanyia mahojiano watahiniwa wa kazi ya mkurugenzi wa kiufundi , huku Marc Overmars wa Ajax – winga wa zamani wa Gunners – na Andoni Zubizaretta wa Marseille wakisemekana kuwa miongoni mwa watahiniwa. (Mail)

Mchezaji wa safu ya ulinzi ya Swansea Ben Cabango, mwenye umri wa miaka 18, anaweza kuwa nyota kijana wa kwanza kabisa wa Uingereza kuongoza kuelekea Ujerumani Germany, huku Muwales anayechezea timu ya vijana walio chini ya miaka -19 akizivutia Bayer Leverkusen na Wolfsburg. (Sun)

Mlinzi wa West Ham Pablo Zabaleta, mwenye umri wa miaka 34, anasema amebakiza michezo miwili kabla ya kuweza kutimiza kipengele katika mkataba wake ambacho kitampatia uwezo wa kusaini mkataba mpya wa kubaki katika klabu hiyo msimu ujao. (Newham Recorder)

Pablo Zabaleta mchezaji wa safu ya ulinzi ya West Ham
Image captionPablo Zabaleta anasema amebakiza michezo miwili ili kutimiza masharti ya kuendelea kubakia kwenye klabu ya West Ham

Southampton inatarajia kuwa mwenyeji wa mashindano ya timu za England zilizofuzu kwa kombe la Euro 2020 dhidi ya Kosovo tarehe 10 Septemba – miaka 17 baada ya St Mary’s mara ya mwisho kuwapokea Three Lions. (Southern Daily Echo)

Timu ya Queens Park Rangers, inayohangaika kuingia katika Ligi ya Championi sambao walimfuta kazi meneja wa zamani wa England Steve McClaren wiki hii, wameazimia kumchukua meneja wa Charlton Lee Bowyer kuchukua kazi hiyo. (Evening Standard)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents