Tupo Nawe

Tetesi za usajili barani Ulaya alhamisi hii, Romero huenda akachukua nafasi ya De Gea endapo akiondoka United, Ole Gunnar amkomalia Rakitic na wengine sokoni

Tetesi za usajili barani ulaya alhamisi hii, Terry, Cancelo, Trippier, Rakitic, Wan-Bissaka na wengine sokoni

Nahodha wa zamani wa England na Chelsea John Terry, ambaye kwa sasa ni naibu meneja wa Aston Villa, anashauriana na Middlesbrough kuhusu uwezekano wa kuwa maneja wao mpya.(Talksport). Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Ureno Joao Cancelo, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa na Juventus kuwa euro milioni 60. (Record – in Portuguese). Atletico Madrid na Napoli wanapania kumsajili beki wa kulia wa Tottenham na mchezaji wa kimataifa wa England Kieran Tripper, 28. (Mirror).

Spurs wameweka dau la £10m kumnunua winga wa Leeds United wa miaka 18, Muingereza Jack Clarke. (Mail)

Manchester United wanashughulikia mpango wa kumsaini Ivan Rakitic, 31, lakini Barcelona wanataka kulipwa uero milioni 48 kumwachilia nyota huyo wa kimataifa wa Croatia. (Record)

Ivan RakiticHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIvan Rakitic

United wanatarajiwa kuwasilisha dau la kwanza la £25m kumunua beki wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka, 21, lakini Eagles wanataka £50m kumwachilia mchezaji huyo. (Evening Standard)

Muargentina Sergio Romero, 32, huenda akapandishwa cheo kuwa kipa wa Manchester United ikiwa David de Gea, 28, ataondoka Old Trafford msimu huu wa joto. (Mail)

United tayari wamewasilisha rasmi ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21. (ESPN)

Everton, West Ham na Manchester United wamepewa nafasi ya kumsaini kwa mkopo kiungo wa kati wa Uholanzi na Marseille Kevin Strootman, 29. (Sky Sports)

Romelu LukakuHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRomelu Lukaku

Antonio Conte anatarajiwa kusajili mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, kutoka Manchester United atakapoajiriwa kama meneja wa Inter Milan. (Times – subscription required)

Liverpool wanakaribia kukamilisha mpangowa £200,000 wa kumsajili kipa raia wa Poland Jakub Ojrzynski, 16, kutoka Legia Warsaw. (Liverpool Echo)

Wolves wanaongoza kinyang’anyiro cha kumsaini mshambuliaji Moussa Marega, 28 rai wa Mali ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £30m-kutoka Porto. (Mirror)

Wales forward Harry WilsonHaki miliki ya pichaBBC SPORT

Newcastle, Southampton na Brighton wote wanataka kusaini winga Harry Wilson, 22, lakini Liverpool wanataka kulipwa £25m kumwachilia nyota huyo wa kimataifa wa Wales. (Sky Sports)

Bournemouth wako tayari kupokea ofa ya kummuuza winga Jordon Ibe, 23 raia wa Uingereza. (Mirror)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW