Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Alhamisi hii, Sancho, Niguez, Griezmann, Moreno, Jovic, Solskjaer, Ake na wengine sokoni

Manchester United ina uwezo wa kumsaka winga wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho mwisho wa msimu huu kwa kuwa klabu yake ya zamani Manchester City haikuweka sheria yoyote ya kumzuia katika kandarasi yake baada ya kumuuza kwamba hafai kuwachezea wapinzani wao (Evening Standard). Dortmund itamwekea Sancho thamani ya £100m na itamwania winga wa Chelsea Callum Hudson Odoi iwapo watataka achukue mahala pake. (Mirror)

Manchester City iko kifua mbele kumsaini kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Uhispania Saul Niguez, 24, this summer. (ESPN)

Barcelona imepunguza moto wao wa kumtaka kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ufaransa Antoine Griezmann kufuatia uvumi kwamba Manchester United itamsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Mirror)

Lazio inakaribia kufikia makubaliano ya kandarasi na beki wa Uhispania mwenye umri wa miaka 26 Alberto Moreno ambaye ataondoka Liverpool mwisho wa msimu huu baada ya kuhudumu kwa miaka mitano katika uwanja wa Anfield.. (Independent)

Barcelona inajiandaa kuwasilisha dau la £43m kumnunua mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic na inatumai kuanza majadiliano na klabu ya Eintracht Frankfurt kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 katika kipindi cha wiki chache zijazo. (Guardian)

Beki wa kulia wa Paris Saint-Germain na Brazil Dani Alves, 35, amekanusha ripoti kwamba amekubali mkataba mpya na mabingwa hao wa ligi kuu ya Ufaransa . (Goal)

Kaimu mkufunzi wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anawataka wachezaji Alexis Sanchez, beki wa Argentina Marcos Rojo, 29, na beki wa kulia wa Ecuado Antonio Valencia, 33, kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu. (Star)

Kiungo wa kati anayeichezea Chelsea kwa mkopo Mateo Kovacic, 24, yuko tayari kujiunga na klabu nyengine ya Uingereza badala ya kurudi katika klabu ya Real Madrid. (Marca)

Chelsea inaweza kumrudisha beki wa Uholanzi na Bournemouth Nathan Ake katika uwanja wa Stamford Bridge huku akivutia timu kama vile Napoli naTottenham. (De Telegraaf – via Caught Offside)

Arsenal itakabiliwa na ushindani mkali kutoka Bayern Munich katika harakati za kumsaka winga wa klabu ya Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe, 23. (Bein Sports – via Mirror)

Bayern Munich wamekubali mkataba na beki wa Atletico Madrid na Ufaransa Lucas Hernandez, 23. (Foot Mercato)

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa anataka kurudi katika ukufunzi mwisho wa msimu huu na kwamba tayari amekataa ofaa ‘tatu’ ama ‘nne’. (Goal)

Manchester City iko tayari kumpatia beki wao wa Ubelgiji na nahodha Vincent Kompany, 32, kandarasi mpya .(Evening Standard)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 32, yuko tayari kurudi nchini Ufaransa ili kupata muda wa kushiriki katika mechi. (Goal)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents