Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya AS Roma wamsaka kwa hali na mali Alexs Sanchez, PSG wamgeukia Dybala

Tetesi za usajili barani Ulaya AS Roma wamsaka kwa hali na mali Alexs Sanchez, PSG wamgeukia Dybala

Roma wamefanya mazungumzo na Manchester United kuhusu uwezekano wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 30. (Telegraph). Wachezaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette, ambao wanadaiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo wanajadiliana kuhusu kurefushwa kwa mikataba yao. (Sun)

Paris St-Germain wanataka kumsaini mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala baada ya uhamisho wa nyota huyo wa miaka 25 kwenda kutibuka. (Mail)

Paulo DybalaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPaulo Dybala

Juventus itaendelea kupokea ofa ya kumuuza Dybala na wako tayari kumkabidhi kiungo huyo kwa klabu yoyote isipokuwa Inter Milan. (Calciomercato)

Kipa wa Manchester United David de Gea bado hajatia saini mkataba mpya baada ya kukubali mkataba mpya wa miaka sita na United mwezi uliopita.(Sun)

Arsenal wako tayari kupokea ofa ya kumuuza beki wa Ujerumani Shkodran Mustafi, 27, na kiungo wa kati wa Misri Mohamed Elneny, 27, kutoka kwa vilabu vya Ulaya. (Evening Standard)

David de GeaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDavid de Gea, Kipa wa Manchester United

Roma wanashauriana na Liverpool kuhusu mkataba wa thamani ya euro milioni 20 (£18.6m) kumhusi beki wa Croatia Dejan Lovren, 30. (Football Italia)

Real Madrid na Barcelona huenda wakamng’ang’ania mshambuliaji wa PSG na nyota wa Brazil Neymar, 27. (AS)

Chelsea wanajiandaa kutumia £200m kuwasajiklili wachezaji wapya mwaka huu wanaposubiri kukamilika kwa marufuku ya uhamisho wa wachezaji waliowekewa na shirikisho la soka Duniani FIFA. (Goal)

NeymarHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNeymar

Chelsea watampatia mkataba mpya mlinzi wa chini wa chini ya miaka 21 Fikayo Tomori, 21, baada ya kupinga uhamisho wake kwenda Everton. (Goal)

Bekiwa Argentina Marcos Rojo, 29, alikuwa tayari kujiunga na Everton kwa mkopo kutoka Manchester United, lakini United wanataka kumuuza. (Liverpool Echo)

Manchester United walikuwa wanatafajkari uwezrkano wa kumsajili mshambuliaji wa Athletic Bilbao wa miaka 25 Mhispania Inaki Williams kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa. (El Chiringuito, via Manchester Evening News)

Marcos RojoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMarcos Rojo (kulia)

Winga wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, atasalia Crystal Palace hadi Januari dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa baada ya mwenyekiti wa klabu hiyo Steve Parrish kusema hatapinga uhamisho wake katika klabu ya Ulaya . (Express)

Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 20, amesema mwaka huu anayetazamia kukabiliana na mchezaji mpya wa Tottenham Mfaransa Tanguy Ndombele, 22 . (Talksport)

Declan RiceHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKiungo wa kati wa West Ham, Declan Rice

Mshambuluaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 28, amekabidhiwa jezi nambari saba ya Real Madrid- iliyovaliwa na Cristiano Ronaldo alipokuwa akichezea klabu hiyo. (Mail)

Mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic alitumia maneno makali kuukosoa mfumo mpya wa michuano ya soka ya ligi ya Major . (ESPN)

Mshambuliaji wa zamani wa Stoke City Saido Berahino, 26, amejiunga na klabu ya Ubelgiji ya Zulte Waregem kwa uhamisho wa bila malipo. (Mail)

Eden HazardHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMshambuluaji wa Ubelgiji, Eden Hazard

Nahodha wa Crystal Palace, Luka Milivojevic ametia saini mkataba mpya wa miaka minne. (Talksport)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents