Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Harry Maguire njiani kutua Man United, Leroy Sane hati hati kutua Bayern Munich na wengine sokoni

Tetesi za usajili barani Ulaya Harry Maguire njiani kutua Man United, Leroy Sane hati hati kutua Bayern Munich na wengine sokoni

Manchester United imeafikiana na Leicester makubaliano ya thamani ya £80m kumsajili Harry Maguire na kumfanya kuwa mlinzi mwenye thamani kubwa katika historia.

United italipa £60m kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 26 – atakayefanyiwa ukaguzi wa kiafya leo Jumatatu – na £20m za ziada katika siku zijazo. (Sun)

Leicester inatarajiwa kuijaza nafasi ya Maguire kwa kumsajili mchezaji wa Brighton Lewis Dunk, baada ya kuafikiana kwa mkataba wa thamani ya £45m kwa mchezaji huyo wa miaka 27. (Sun)

Celtic imekataa ombi la Arsenal la hivi karibuni linalokisiwa kuwa na thamani ya £25m – ili kumsajili beki wa kushoto mwenye miaka 22 Kieran Tierney. (Sky Sports)

Manchester City inaamini Leroy Sane ataisusia Bayern Munich iwapo itawasilisha ombi la kumsajili winger huyo wa Ujerumani mwenye miaka 23. (Daily Mirror)

Tottenham na Arsenal zimejiunga na Manchester City katika kumfukuzia beki kamili wa Brazil Dani Alves mwenye umri wa miaka 36, ambaye ni ajenti huru tangu alipoondoka Paris St-Germain. (Mundo Deportivo kupitia Daily Mail)

Dani AlvesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTottenham na Arsenal zimejiunga na Manchester City katika kumfukuzia beki kamili wa Brazil Dani Alves

Atletico Madrid haina ushahidi wa kuthibitisha tuhuma kwamba Barcelona ilikuwa na makubaliano tayari na mchezaji wa kiungo cha mbele wa Ufaransa Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 28, mapema mwezi Machi, kwa mujibu wa rais wa Barca Josep Maria Bartomeu. (Goal)

Mchezaji anayelengwa na Arsenal, Everton mwenye umri wa miaka 23 anayeichezea Gremio, anasema amepewa pendekezo lakini amekataa kufichua jina la klabu iliyomfuata. (Mirror)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema klabu hiyo itaendelea kuweka wazi matumaini yake kuhusu kumsajili beki wa kushoto kuichukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uskotchi Andrew Robertson, mwenye umri wa miaka 25, wakati wa dirisha la uhamisho msimu wa joto. (ESPN)

KloppHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Aliyekuwa winga wa Newcastle Chris Waddle anaamini kuidhibiti Magpies itakuwa changamoto kubwa katika miaka 21 ya usimamizi wa Steve Bruce iwapo ataondoka Sheffield Jumatano kuelekea St James’ Park. (Newcastle Chronicle)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Herbie Kane, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa mkopo kwenda katika klabu ya ubingwa wiki hii. Brentford, Charlton na Hull zote zinataka kumsajili mchezaji huyo wa miaka 20 aliyeichezea Doncaster msimu ulioipita. (Goal)

Bora za Jumapili 14.07.2019:

CoutinhoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBarcelona ilimsajili Coutinho kutoka Liverpool kwa pauni milioni 142 Januari 2018

Kiungo wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, atakataa ofa ya kujiunga na Manchester United, akiwa na malengo ya kuelekea klabu Paris St-Germain, japo anaweza pia kukubali kurejea Liverpool.(Express)

Barcelona wamemuhakikishia wakala wa Coutinho kuwa hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo, japo anadai kuwa mteja wake anawekwa sokoni na wawakilishi walio karibu kabisa na klabu hiyo. (Sky Sports)

Liverpool pia wamejiunga kwenye mbio za kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji wa CSKA Moscow Fedor Chalov mwenye thamani ya pauni milioni 20. Arsenal, Manchester City, Tottenham, Chelsea na Manchester United pia wanamnyemelea mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Mirror)

Mchezaji ghali zaidi duniani wa Paris St-Germain, Neymar, amekoleza uvumi kuwa anarudi Barcelona baada ya kuachia video anayoonekana amevaa jezi ya Barca, pamoja na mistari ya biblia yenye mafumbo. (Goal.com)

Neymar akiwa Barcelona
Image captionNeymar alijiunga na PSG kutoka Barcelona kwa dau lililovunja rekodi la pauni milioni 200 mwaka 2017

Bayern Munich hawatakata tamaa ya kumsajili mshambuliaji kinda wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 18, huku wakitarajiwa kutangaza dau la pauni milioni 45 wiki hii. (Mail)

pOGBA

Manchester United hawatamuuza kiungo Mfaransa Paul Pogba kwenda Real Madrid iwapo miamba hiyo ya Uhispania watawasilisha ofa yao baada ya dirisha la usajili kufungwa kwa upande wa England, Agosti 8. (Mirror)

Beki wa Leicester na England Harry Maguire, 26 – ambaye anahusishwa na uhamisho kwenda Man United kwa dau la £75m – ameambia klabu yake kuwa anataka kuondoka. (Mail)

Maguire
Image captionMaguire ametia nia ya kuihama Leicester kwenye dirisha hili la usajili

Maguire ameishutumu Leicester kwa kumkadiria kwa dau ghali ili asinunulike. Tayari klabu hiyo imeshazikataa ofa za pauni milioni 70 kutoka kwa United na City. (Sun)

Kiungo mchezeshaji wa Tottenham na timu ya taifa ya Denmark Christian Eriksen, 27, yawezekana akaendelea kusalia kwenye klabu hiyo ya jijini London baada ya kuwa na uhaba wa klabu ambazo zimeonesha nia ya kumsajili. (Guardian)

Mane Sadio
Image captionSadio Mane kung’oka Liverpool?

Liverpool hawajafanya mazungumzo yoyote na Real Madrid juu ya mshambuliaji raia wa Senegal Sadio Mane, 27, licha ya mkuu wa chama cha soka cha Senegal Saer Seck kudai kuwa Madrid wamepeleka ofa ya usajili. (Liverpool Echo)

Kiungo wa Everton na Senegal Idrissa Gueye, 29, amesema anafahamu juu ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho kwenda PSG lakini kwa sasa amedai malengo yake yapo AFCON. (Sport Witness)

Arsenal wapo Tayari kuminyana na Tottenham na Juventus katika mbi za kumsajili kiungo waklabu ya Roma ya Italia Nicolo Zaniolo, 20. (Calciomercato)

Liverpool pia wamejiunga kwenye mbio za kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji wa CSKA Moscow Fedor Chalov mwenye thamani ya pauni milioni 20. Arsenal, Manchester City, Tottenham, Chelsea na Manchester United pia wanamnyemelea mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Mirror)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents