Tupo Nawe

Tetesi za usajili barani ulaya Ijumaa hii, Bale, Herrera, Gomes, Zouma, Varane na wengine sokoni

Arsenal wanatariwa kuingia katika harakati za kumsajili kiungo wa Manchester United Ander Herrera, 29, kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu, na kupigana vikumbo na PSG juu ya saini ya Mhispania huyo. (L’Equipe, via Express). Kocha wa Everton Marco Silva ametangaza kuwa huenda akawasjili moja kwa moja beki Kurt Zouma, 24 kutoka Chelsea, na kiungo Andre Gomes, 25 kutoka Barcelona – ambao wote wapo kwa mkopo klabuni hapo. (Liverpool Echo)

Silva pia amesema wala hajali uvumi unaoendelea kuwa kiungo tegemezi wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Senegal Idrissa Gueye, 29, kuwa atajiunga na Manchester United mwishoni mwa msimu. (Manchester Evening News)

Real Madrid wanataka kulipwa kitita cha pauni milioni 112 ili kumuachia mshambuliaji wao raia wa Wales Gareth Bale, 29, mwishoni mwa msimu huu. Madrid wanaamini vilabu vikubwa vya Uingereza vitakuwa radhi kulipa fedha hizo. (AS)

Gareth Bale
Image captionGareth Bale (kushoto) amekuwa na wakati mgumu na Real Madrid.

Wakati huo huo, United wanapigiwa upatu kumsajili kiungo fundi wa klabu ya Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 24, mwishoni mwa msimu. (A Bola, via Mail)

Real Madrid hawatakubali kumuachia beki wao wa kati Raphael Varane, 25, kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu pasi na kutolewa kitita cha pauni milioni 431. (AS)

Burnley wapo tayari kupokea ofa za usajili kwa kipa wao Nick Pope, 26, na Bournemouth wanapigiwa chapuo la kumnasa kipa huyo. (Mail)

Verane vs Messi
Image captionVerane (kulia) akipambana na Leo Messi kwenye mchezo wa el classico .

Wachezaji wa Bayern Munich mshambuliaji Robert Lewandowski, 30, na winga Kingsley Coman, 22, walipigana wakiwa mazoezini Alhamisi asubuhi (Bild – in German)

Arsenal wanataka kumsajili kiungo wa Ufaransa Christopher Nkunku, 21, ambaye amegoma kuongeza mkataba na klabu ya PSG. (Le Parisien – in French)

Klopp
Image captionKlabu ya Liverpool ambayo inaongozwa na kocha Jurgen Klopp ipo mbioni kusaini mkataba mnono na kampuni ya Nike.

Liverpool wapo kwenye mazungumzo ya kina na kampuni ya Nike kwa ajili ya mkataba wa utengenezaji wa jezi zao ambao thamani yake utazidi hata ule wa Manchester United na Adidas wa pauni milioni 750. Iwapo mkataba wa Liverpool utasainiwa utakuwa ndiyo mkubwa zaidi kwenye historia ya Ligi ya Premia. (ESPN FC)

Manchester United wamempa ofa ya mkataba wa miaka minne kipa kinda wa klabu ya Marseille Mfaransa Ahmadou Dia, 20. (L’Equipe, via Metro)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW