Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Ijumaa hii, Eriksen, Alaba, Anderson, Higuain, Neymar, Icardi, Dybala na wengine sokoni

Hatua ya Real Madrid kumnyatia mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 27, huenda ikasababisha msururu wa uhamisho ikiwemo ule wa mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, 25, kuelekea Atletico Madrid. (Calcio Mercato) Mchezaji wa Tottenham Christian Eriksen, 27, amehusishwa na uhamisho wa klabu ya Real Madrid. (talksport)

Beki wa Bayern Munich David Alaba, 26, amefichua kuwa alikuwa shabiki mkubwa wa Arsenal alipokuwa mtoto na kutoa ishara kwamba angependelea kuondoka katika uwanja wa Allianz Arena. (Bild via Daily Mail).

Winga wa West Ham Felipe Anderson, 25, ndio mchezaji mbadala anayelengwa na Real Madrid kwa dau la £65m iwapo klabu hiyo itashindwa kumvutia nyota wa Ubelgiji Eden hazard kutoka Chelsea (Sky Sports)

AC Milan imeanzisha mazungumzo na klabu ya Cagliari kuhusu kiungo wa kati wanayemthamini sana Nicolo Barella, 22. (Sky Italia via Sempre Milan)

Chelsea inafikiria kusitisha mkopo wa raia wa Argentina Gonzalo Higuain mwisho wa msimu huu ikimaanisha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 atarudi Juventus. (marca)

Manchester City ina matumaini ya kumsaini kinda wa Benfica Ronaldo Camara. (Evening Standard)

Manchester United inafikiria kumnunua nahodha wa klabu ya Sporting Lisbon na Portugal Bruno Fernandes, 24. (Star – via Manchester Evening News)

Inter iko tayari kushindana na Everton kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona na Portugal Andre Gomes. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Goodison Park. (sport)

Mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi huenda akaondoka katika uwaja wa San Siro kwa dau la £43.4m huku Real Madrid na Juventus zikiwa na hamu ya mchezaji huyo mwenye umri wa 26. (marca)

Liverpool haitasitisha makubaliano ya mkopo wa kipa wa Ujerumani Loris Karius’ katika klabu ya Besiktas na kumrudisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 uwanjani Anfield. (mirror)

Liverpool haitatumia kitita kikubwa cha fedha katika dirisha la uhamisho mwisho wa msimu huu. (Liverpool Echo)

Ajenti wa beki wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar 24, amedai kwamba klabu za Real Madrid na Barcelona zina hamu ya kumsaini mteja wake.. (goal)

Rais wa klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness anasema kuwa mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola husafiri ili kukutana na mmiliki wa klabu hiyo Sheikh Mansour na kumuonyesha kanda za video za wachezaji anaowalenga katika uhamisho ili kuweza kununua wachezaji hao. (goal)

Fenerbahce inatumai kwamba beki wa Leicester na Uturuki Caglar Soyuncu, 22, atarudi Uturuki kwa mkopo msimu ujao. (Leicester Mercury)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents