Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumamosi hii, Greizman anukia Man United, De Gea aanza kulegesha masharti kwa Ole Gunnar, Ramos ,Mkhitaryan, Terry, Welbeck na wengine sokoni

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumamosi hii, Greizman anukia Man United, De Gea aanza kulegesha masharti kwa Ole Gunnar, Ramos ,Mkhitaryan, Terry, Welbeck na wengine sokoni

Manchester United wako mbioni kumsaini mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann, baada ya tetesi zanazotilia shaka uhamisho wa nyota huyo wa miaka 28 kwenda Barcelona kuibuka. (Independent)

United pia wanajiandaa kuweka dau la kumnunua nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos, 33, ambaye huenda akaondoka msimu ujao baada ya kujiunga na klabu hiyo miaka 14 iliyopita. (Mail)

Arsenal wako tayari kumuuza Henrikh Mkhitaryan, 30, msimu ujao licha ya kuunga mkono hatua ya kiungo huyo raia wa Armenia kujiondoa katika fainali ya ligi ya Europa itakayochezwa nchini Azerbaijan wiki ijayo kwa kuhofia usalama wake.

Mkhitaryan aliifungia Arsenal mabao 25 katika ligi kuu wa England msimu wa mwaka 2018-19. (Sun)

Henrikh MkhitaryanHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHenrikh Mkhitaryan

Kiungo wa kati wa Chelsea, Mhispania Marcos Alonso, 28, huenda akaondoka Stamford Bridge licha ya kusaini mkataba wa miaka mitanio na klabu hiyo mwezi Oktoba mwaka jana. (Evening Standard)

Huku hayo yakijiri, Mshambuliaji wa The Blues na Ubelgiji Eden Hazard, 28, anataka mchakato wa uhamisho wake kwenda Real Madrid ukamilishwe kufikia tarehe 4 mwezi Juni, lakini klabu hiyo bado haijafanya maamuzi kwasababu inahofia kupoteza £26m. Real imetoa ofa ya £86m na wanataka karibu £112m kumuachilia nyota huyo. (Mirror)

Kipa wa Uhispania na Manchester United David de Gea, 28 anakaribia kutia saini mkataba mpya na klabu hiyo, japo mkataba wake wa sasa unakamilika msimu ujao

De Gea,ambaye alijiunga na United tangu mwaka 2011, anaweza kutia saini masharti ya awali ya kujiunga na vilabu vya kigeni kuanzia mwezi Januari mwaka 2020. (Sky Sports)

David de GeaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDavid de Gea

Everton wanapania kusajili mshambuliaji wa Arsenal na England Danny Welbeck, 28, katika uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Evening Standard)

Napoli Crystal Palace, West Ham na Bournemouth wamevutiwa na mlinzi wa Liverpool na England Nathaniel Clyne, 28.

Atletico Madrid na Valencia wanawania kumsaini kwa mkopo mchezjai mahiri wa Monaco,Radamel Falcao ambaye pia aliwahi kuwa mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Chelsea.

Nyota huyo raia wa Colombia aliye na umri wa miaka 33 pia alichezea Atletico kwa misimu miwili kati ya mwaka 2011 na 2013. (L’Equipe – in French)

Radamel FalcaoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRadamel Falcao, mshambuliaji wa zamani wa Manchester United

Meneja wa zamani wa Chelsea na Tottenham Andre Villas-Boas, 41, anakaribia kuteuliwa kocha wa Marseille.

Siku ya Jumatano Rudi Garcia alitangaza uamuzi wake wa kuondoka klabu hiyo ya Ligue 1 club mwisho wa msimu huu. (Telegraph)

Mlinzi wa zamani wa Arsenal na England Sol Campbell, 44, hajalipwa kwa miezi miwili na klabu ya Macclesfield inayocheza soka ya daraja la pili. Campbell, hata hivyo amesema hana nia ya kuhama klabu hiyo. (Sun)

Sol CampbellHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSol CampbellChanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents