Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumamosi hii, Sterling, Courtois, Rodriguez, Giroud, Suso, Umtiti, na wengine sokoni

Real Madrid ina mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 24, kama sehemu ya kuimarisha kikosi chake. (Mirror). Meneja wa Real Zinedine Zidane amemuonya kipa wa klabu hiyo Mbelgiji Thibaut Courtois, 26, kuhusiana na utendakazi wake mbaya siku za hivi karibuni. (Sun)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amefutilia mbali uwezekano wa klabu hiyo kuwasajili wachezaji wapya. Badala yake Klopp ameongeza kuwa mpango weka ni kuimarisha timu iliyopo sasa kufikia kiwango cha juu zaidi cha uchezaji kwa 100% . (Mail)

Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, 34, huenda akachukuliwa hatua na Uefa baada ya kuonekana kana kwamba anawwapia mashabiki wa Atletico Madrid wakati wa mechi ya ligi ya mabingwa. (La Gazzetta dello Sport – in Italian)

Mlinzi wa Ufaransa Samuel Umtiti, 25, amesema kuwa angelipendelea kujiunga na Manchester City ama Manchester United ikiwa ataondoka Barcelona msimu huu. (Calciomercato – in Italian)

Mshambuliaji wa Chelsea, mfaransa Olivier Giroud, 32, amesema haoni uwezekano wake wa kuendelea kuchezea klabu hiyo endapo ataendelea kucheza nafasi yake ya sasa. (Sun)

Meneja wa Muda wa Manchester United Ole Gunner Solskjaer ameamua ni wachezaji gani wataondoka Old Trafford msimu huu wa joto, huku beki wa kulia Antonio Valencia,33 akiwa na uhakika wa kuondoka kwake. (Manchester Evening News)

Arsenal inaaminiwa kuwa moja ya vilabu vinavyopania kumsajili Valencia, baada ya baba yake kuthibitisha kuwa mchezaji huyo atahama Manchester. (Metro)

Gunners wako katika hatari ya kumkosa mkurugenzi wa zamani wa kiufundi wa Roma, Monchi, baada ya klabu ya La Liga, Sevilla, kufanya mazungumzo na mhispania huyo wa miaka 50. (Metro)

Monchi (Kushoto) Mkurugenzi wa kiufundi wa zamani wa Roma

Arsenal pia inaongoza katika kinyan’ganyiro cha usajili wa mshambuliaji wa AC Milan, raia wa Uhispania Suso, 25. (Mirror)

Meneja wa Newcastle, Rafaeal Benitez amedokeza kuwa ana matumaini ya kumshawishi kiungo wa kati Isaac Hayden asihame klabu hiyo. Tayari kiungo huyo wa miaka 23 ameomba kupewa uhamisho mara mbili. Benitez ana amini mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal ana nafasi nzuri ya kuchezea timu ya taifa ya England. (Chronicle)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.


Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents