Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumanne hii, Coutinho, Rashford, Pogba, Mane, Hazard, Benitez, Vieira na wengine sokoni

Real Madrid ina mipango miwili ya uhamisho-mmoja ukishirikisha kumsaini mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard mwenye umri wa miaka 28 mbali na kuwachukua kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba na mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane mwenye umri wa miaka 27. (El Confidencial – in Spanish)

Manchester United wamemwambia ajenti wa Pogba Mino Raiola kwamba Real Madrid italazimika kulipa Yuro milioni 150 ili kumsaini mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa 26. (Marca)

Kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, 26, huenda akalengwa na Chelsea iwapo marufuku ya uhamisho ya Chelsea itaondolewa mwisho wa msimu lakini mchezaji huyo amekataa uhamisho wa kuelekea Manchester United. (Sport)

Phillipe Coutinho

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alikataa kuzungumzia hatma ya Coutinho wakati wa mkutano na vyombo vya habari wakati wa maandalizi ya kikosi chake katika mechi ya awamu ya pili ya robo fainali dhidi ya Barcelona. (Manchester Evening News)

Barcelona itajaribu kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford kwa dau la £100m. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ana mwaka mmoja katika mkataba wake na bado hajaongeza. (Mirror)

Manchester United imejiandaa kulipa £31m kumsaini beki wa Roma na Ugiriki Kostas Manolas, 27. (Leggo, via Sun)

Rafael Benite

Newcastle United inatumai kuafikia makubaliano na mkufunzi Rafael Benitez kuhusu nyongeza ya kandarasi yake katika kipindi cha wiki mbili zijazo. (Newcastle Chronicle)

Mchezaji wa zamani wa Arsenal na Ufaransa Patrick Vieira ni mmojawapo wa wawaniaji wa kazi ya ukufunzi katika klabu ya Lyon. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 42 kwa sasa anafunza klabu ya Nice. (Le Parisien, via Sun)

Inter Milan ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, 28. (Tuttosport, via Calciomercato)
Image captionInter Milan ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, 28. (Tuttosport, via Calciomercato)

Nahodha wa klabu ya Manchester City Vincent Kompany anasema kuwa atakuwa katika klabu hiyo msimu ujao. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 anakamilisha kandarasi yake mwisho wa msimu huu . (Talksport)

Inter Milan ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, 28. (Tuttosport, via Calciomercato)

Manchester United, Juventus na Paris St-Germain zinafikiria kumsaini kiungo wa kati wa klabu ya Sporting Lisbon na Ureno ,24, Bruno Fernandes. (A Bola, via Mail)

Joao Felix

Hatma ya kiungo wa kati wa Southampton Jody Clasie katika klabu hiyo haijulikani. Raia huyo wa Uhalonzi ,27, yuko kwa mkopo katika klabu ya Feyenoord na alitarajiwa kujiunga nao kwa mkataba wa kudumu lakini haelewani na mkufunzi Giovanni van Bronckhorst. (Independent)

Maafisa wa Juventus watakutana na Benfica siku ya Jumanne ili kuzungumzia uhamisho wa mshambuliaji Joao Felix ambaye anataka kucheza na nyota mwenza wa Ureno Cristiano Ronaldo. (AS)

Joao Felix

Mshambuliaji wa Newcastle United Dwight Gayle, 29, anasema kuwa huenda akaichezea West Brom msimu ujao ambapo mchezaji huyo wa Uingereza yupo kwa mkopo. (Shields Gazette)

Arsenal huenda ikamzuia mchezaji wa Algeria mwenye umri wa miaka 21 kutonunuliwa huku akidaiwa kuvutia klabu kama vile Empoli. (Le10 Sport, via Mirror)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents