Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumanne hii, Hazard, Eriksen, Solskjaer, Gundogan, De Light, Jokanaovic na wengine sokoni

Zinedine Zidane amerejea tena Real Madrid miezi kumi baada ya kuondoka klabu hiyo. Miamba hao wa soka wanapania kuwasajili wachezaji kadhaa ikiwa ni pamoja na mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 28, na kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27. (Independent)

Zinedine Zidane aliichezea Real Madrid kati ya mwaka 2001 na 2006 na baadae akaiongoza klabu hiyo kuanzia mwaka 2016 hadi 2018.

Gareth Bale, 29, na Luka Modric, 33, ni miongoni mwa wachezaji wanaojiandaa kuondoka uwanjwa wa Bernabeu msimu huu wa joto. (Independent). Manchester United huenda ikamuidhinisha Ole Gunnar Solskjaer kuwa meneja wao. Mshambuliaji huyo wa zamani wa miaka 46, sasa ni mmoja wa watu wanaowania nafasi hiyo. (Mirror)

Ilkay Gundogan, 28, amesema hatalazimishwa na Manchester City kutia saini mkataba mpya japo hakupinga uwezekano wake wa kuondoka klabu hiyo msimu huu wa joto. (Telegraph)


Ilkay Gundogan aliiwakilisha Manchester City mara 15 msimu uliyopita

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu anajiandaa kuimarisha mpango wake wa kumsaini mlinzi wa Ajax Matthijs de Ligt, 19. (Goal.com)

Viongozi wa klabu ya Arsenal wamesema wachezaji ambao wamesalia na miaka miwili kabla ya mikataba yao kuisha na wamekataa kusaini mkataba mpya watauzwa. Kiungo wa kati wa Gunners Aaron Ramsey, 28, ataondoka klabu hiyo bila malipo mwisho wa msimu huu, huku Arsenal ikuwa makini isirudie hali hiyo siku zijazo. (Metro)


Ramsey ameshinda kombe la FA Cup mara tatu na Community Shield mara moja akiwa Arsenal

Maafisa wa Arsenal wameonekana tena wakimfuatilia kiungo wa kati wa AC Milan ambaye aliwahi kuichezea Liverpool, Suso, 25. (Caught Offside)

Meneja wa England Gareth Southgate anatafakari uwezekano wa kumrudisha kikosini kiungo wa kati wa Southampton James Ward-Prowse, 24 baada ya mchezaji huyo kuimarika.
Southgate, Jumatano hii anatarajiwa kutangaza kikosi chake kitakachoshiriki michuano ya kufuzu kwa kombe la Euro mwaka 2020 dhidi ya Czech Republic na Montenegro. (Mirror)

Celtic inataka kumsajili mlinzi wa Chelsea omas Kalas, 25, kwa euro milioni tano lakini hilo lisipowezekana wana mpango wa kumchukwa mlizi wa Red Star Belgrade, Srdjan Babic, 22. (Star)

Liverpool, Tottenham, Manchester United, Bayern Munich, Borussia Dortmund na Inter Milan wote wanamnyatia winga wa PSV Eindhoven Steven Bergwijn, wa miaka 21 ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa zaidi ya £30m. (De Telegraaf, via Team Talk)

Meneja wa Besiktas, Senol Gunes amekiri kuwa mkopo wa miaka miwili wa kipa wa Liverpool goalkeeper Loris Karius, 25, “haukufanya kazi” na kudokeza kuwa watamtema wakipata kipa mwingine mzuri. (Liverpool Echo)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents