Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumanne hii, Ozil, Hazard, Arnautovic, Higuain, Morata na wengine sokoni

Chelsea itaomba £100m iwapo mchezaji raia wa Ubelgiji Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 28, ataiambia klabu kwamba anataka kujiunga na Real Madrid. (Telegraph)

Meneja wa Arsenal Unai Emery anaridhia kumruhusu mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil, mwenye umri wa miaka 30, kuondoka katika klabu hiyo ili kuweza kuwasajili wachezaji wawili wapya. Kwa sasa Ozil ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi Arsenal katika mkataba wenye thamani ya £350,000 kwa wiki. (Mail)

Mshambuliaji wa West Ham raia wa Austria Marko Arnautovic, mwenye umri wa miaka 29, atakamilisha uhamisho wa thamani ya £35m kwenda katika timu ya ligi kuu ya China Shanghai SIPG kabla ya mwisho wa wiki. (Sun)

Hammers itamlenga mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson, mwenye umri wa miaka 26, iwapo watamruhusu Arnautovic kuondoka mwezi huu. (Sky Sports)

Sevilla imevunjika moyo kumsajili mshambuliaji wa Chelsea raia wa Uhispania Alvaro Morata, mwenye umri wa miaka 26, kutokana na gharama yake kubwa, na baada ya kukataliwa pendekezo lao la thamani ya £40m. (Evening Standard)

Morata yu tayari kupokea kato la mapato ili kujiunga na Atletico Madrid, itakayohitaji kumuuza mchezaji mwingine ili kuweza kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid. (Marca)

Wachezaji wa Manchester United wanaendelea kushinikiza meneja wa mpito Ole Gunnar Solskjaer apewe mkataba wa kudumu mwishoni mwa msimu. (Telegraph)

Solskjaer anataka kumuondoa Marouane Fellaini na huenda akamruhusu mchezaji huyo wa kiungo cha kati mwenye miaka 31 raia wa Ubelgiji aondoke kwa mkopo mwezi huu Januari. (Talksport)

Kocha huyo raia wa Norway ameshauriana na meneja wa zamani Sir Alex Ferguson kuhusu uteuzi wa timu tangu apokee mikoba kutoka kwa meneja aliyefutwa kazi Jose Mourinho. (Manchester Evening News)

Chelsea wamekubali makubaliano binafsi na mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Argentina Leandro Paredes, aliye na miaka 24, na wamewasilisha ombi la thamani ya £27m kwa Zenit St Petersburg. (Mirror)

Liverpool, Tottenham na Everton ni miongoni mwa vilabu katika ligi ya England walio na hamu ya kusmajili winga wa Uholanzi Arnaut Danjuma Groeneveld, aliye na miaka 21, kutoka Club Brugge. (Mail)

Juventus na AC Milan itafanya mazungumzo kuhusu azma ya mshambuliaji mwenye miaka 31 Gonzalo Higuain kutaka kujiunga na Chelsea. Mchezaji huyo amechukuliwa kwa mkopo na Milan kutoka timu bingwa katika Serie A, Juve. (Evening Standard)

Mabingwa wa Ligue 1 Paris St-Germain wanahitaji mchezaji wa kiungo cha kati mlinzi na wanamlenga mchezaji wa Everton na timu ya taifa ya Senegal Idrissa Gueye, mwenye umri wa miaka 29. (L’Equipe)

Lakini timu hiyo ya Toffees wamemuambia Gueye watapokea maombi tu yenye thamani ya £40m kumuuza katika dirisha la uhamisho Januari. (Mirror)

Wolves wana hamu ya kumsajili beki wa kulia wa Stoke Moritz Bauer, kwa mkopo kwa msimu uliosalia. (Express and Star)

West Ham imeanzisha mazungumzo kuhusu kumsajili mlinzi anayepigiwa upatu wa Bristol Rovers Michael Kelly, aliye na miaka 21. Mkataba wa mchezaji huyo wa Uskotchi unamalizika mwishoni mwa msimu. (Football Insider)

Mchezaji kiungo cha kati wa Ajax na Uholanzi Frenkie de Jong, mwenye miaka 21, anakaribia kujiunga na PSG kwa thamani ya takriban £67m, na kupokea malipo ya £7m kwa mwaka. (AS)

Mshambuliaji wa Japan Shinji Okazaki, mwenye miaka 32, anataka kuondoka Leicester mwezi wa Januari kutokana na kutojumuishwa katika kikosi cha kwanza. (Sky Sports)

Everton inajitayarisha kumhamisha mshambuliaji raia wa Uhispania anayeichezea Espanyol Borja Iglesias, mwenye miaka 25, aliye na kifungu cha thamani ya £25m katika mkataba wake kuruhusu kuuzwa. (Sun)

Lakini Iglesias amekataa pendekezo hili na ameweka bayana kwamba hataki kuondoka Espanyol kati kati ya msimu. (Marca)

Marseille bado ina hamu ya kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Nice Mario Balotelli, mwenye miaka 28, lakini wameshindwa kukubaliana mshahara na mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City. (L’Equipe)

Uhariri katika gazeti la Uhispania Marca umemshauri mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid Isco kuwabadili wawakilishi wake katika vyombo vya habari au ahatarishe kuiangamiza taaluma yake Bournemouth. (Marca)

Chanzo BBC,

By Ally Juma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents