Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumanne hii, Pogba, Mbappe, Mane, Neymar, Felix, Umtiti na wengine sokoni

Kiungo Mfaransa Paul Pogba, 26, amefikia maamuzi ya kuihama Manchester United mwishoni mwa msimu na anafikiria kwenda Ligi ya Uhispania ama Italia. (AS – in Spanish)

Mshambuliaji wa Liverpool na Senegali Sadio Mane, 26, pia anatakiwa na Real Madrid mwishoni mwa msimu. (Marca – in Spanish)

Mshambuliaji wa Brazil Neymar yumo katika mazungumzo ya kuongeza mkataba na klabu yake ya Paris St-Germain, kwa mujibu wa baba wa mchezaji huyo. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 amekuwa akihusishwa na mipango ya kuhamia Real Madrid. (ESPN)

Benfica wanataka kuongeza kipengele kigumu kwenye mkataba wa mshambuliaji Mreno Joao Felix ili kuzipunguza makali klabu ambazo zinzmnyemelea mshambuliaji kinda huyo. Manchester United na Juventus zimekuwa zikihusishwa na kumtaka Felix, 19. (Tuttosport – in Italian)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ameazimia kumsajili Mshambuliaji kinda wa Ufaransa na klabu ya Paris St-Germain Kylian Mbappe, 20, kwa udi na uvumba, na yupo tayari kutangaza dau nono la pauni milioni 240. (France Football – in French)

Barcelona wanaweza wakawauzia Manchester United mlinzi wao wa kati Samuel Umtiti mwishoni mwa msimu, japo beki huyo mwenye miaka 25 anataka kusalia Camp Nou. (Mail)

Beki wa Chelsea Christensen amesema kuwa wachezaji wa klabu hiyo wametaarifiwa kuwa hawataruhusiwa kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu endapo marufuku ya usajili inayoikabili klabu hiyo haitaondoshwa. (Times)

Kiungo wa Manchester United raia wa Serbia Nemanja Matic amesema nataka kocha wa mpito wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer pamoja na benchi lake lote la ufundi wapewe kazi ya kudumu katika klabu hiyo. (ESPN)

Kiungo wa Manchester United raia wa Uhispania Ander Hererra, 29, amesema ni jambo la kawaida kuhusishwa na kutaka kuhamia klabu ya Paris St-Germain kutokana na kusalia miezi mitatu tu mpaka mkataba wake na Old Trafford kufikia tamati. (El Periodico – in Spanish)

Arsenal pia wanataka kumsaini Hererra kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu. (Mail)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents