Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumanne hii, Rice, Pogba, Adams, Clyne, Acosta, Carroll na wengine sokoni

Manchester United kutangaza dau la usajili la pauni milioni 50 ili kumnasa kiungo kinda wa West Ham Declan Rice,20. (Irish Independent). Rice, amesema kujiunga na West Ham ulikuwa uamuzi bora kabisa aliowahi kuufanya baada ya Chelsea kumtema akiwa na miaka 14. (Standard)

LONDON, ENGLAND – SEPTEMBER 29: Declan Rice of West Ham United and Paul Pogba of Manchester United during the Premier League match between West Ham United and Manchester United at London Stadium on September 29, 2018 in London, United Kingdom. (Photo by Arfa Griffiths/West Ham United via Getty Images)

Beki wa kushoto wa Ajax Nicolas Tagliafico, 26, amesema kuwa mwisho wa msimu huu utakuwa ni muda muafaka wa kuhamia kwenye Ligi ya Premia. Beki huyo raia wa Argentina anawindwa na Arsenal. (Mirror)

Kocha msaidizi wa Manchester United Mike Phelan amesema kiungo wa klabu hiyo Paul Pogba, 26, “bado hajamaliza kazi yake” na anamtaka mchezaji huyo kusalia Old Trafford. (Telegraph)

Paul Pogba
Image captionPaul Pogba anaendeleakugonga vichwa vya habari akihusianishwa na uhamisho kwenda Real Madrid mwishoni mwa msimu.

Jarida la ‘France Football’ la nchini Ufaransa klinamshawishi Pogba kuhama Old Trafford na kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu. (France Football – in French)

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amesema klabu yake ilitaka kumsajili Pogba kutokea Juventus lakini ilishindwa kufikia dau la United mwaka 2016. (ESPN)

Che Adams
Image captionChe Adams

Everton wanajiandaa kutangaza dau la usajili ili kumnasa mshambuliaji wa Birmingham City Che Adams, 22. (Football Insider)

West Ham hawatampatia Andy Carroll, 30, mkataba mpya mwishoni mwa msimu. Mshambuliaji huyo amefanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu, hali inayomfanya kushindwa kurejea dimbani mpaka msimu utakapokwisha. (Mail)

Andy Caroll
Image captionAndy Caroll kutemwa na West Ham mwishoni mwa msimu.

Wagonga nyundo hao wa London watapambana na Bournemouth ili kumsajili beki wa Liverpool Nathaniel Clyne, 28. Clyne yupo kwa mkopo Bournemouthtoka mwezi Januari. (Goal)

Kiungo wa DC United na Argentina Luciano Acosta, 24, amesema kuwa ana furaha kunyemelewa na Manchester United.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents