Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumanne hii, Sane, Pogba, Conte, Batistuta, Giroud na wengine sokoni

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumanne hii, Sane, Pogba, Conte, Batistuta, Giroud na wengine sokoni

Bayern Munich wanaamini kuwa watamsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ujarumani Leroy Sane, 23, kutoka Manchester City msimu huu wa joto. (Mirror). Manchester United wanatarajiwa kuitisha euro milioni 160 (£138m) kumuuza kiungo wa kati wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba, 26. (Star).

MANCHESTER, ENGLAND – NOVEMBER 11: Paul Pogba of Manchester United greets Leroy Sane of Manchester City before during the Premier League match between Manchester City and Manchester United at Etihad Stadium on November 11, 2018 in Manchester, United Kingdom. (Photo by Manchester City FC/Man City via Getty Images)

Mlinzi wa Leicester na nyota wa kimataifa wa England Harry Maguire, 26, ni mmoja wa walinzi wa kati wanaolengwa na Manchester City kuchukua nafasi ya Vincent Kompany. (Sky Sports)

Paul PogbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPaul Pogba

Meneja mpya wa Anderlecht, Kompany anamfuatilia kwa karibu kocha wa chuo mpira cha Manchester City, Simon Davies na mkuu wa sayansi ya michezo Sam Erith, kuungana nae mjini Brussels. (Telegraph)

Meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ameafiki masharti ya kujiunga na Inter Milan kama kocha wao mpya msimu ujao. (Guardian)

Juventus wameachana na Conte na sasa wanamlenga meneja wa sasa wa Chelsea, Maurizio Sarri. (Sun)

Antonio ConteHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAntonio Conte

Arsenal wametoa ofa ya kumnunua kipa wa valencia Mbrazilia Norberto Murara, baada ya kuzungumzana wawakilishi wa mchezaji huyo wa miaka 29. (Star)

Nyota wa zamani wa kimataifa wa Argentina Gabriel Batistuta, 50, bado hajafikia kiwango cha ukufunzi wa timu kubwa lakini sasa inaaminiwa kuwa ameonesha nia ya kuchukua nafasi ya usimamizi iliyoachwa wazi katika klabu ya Middlesbrough. (Hartlepool Mail)

Chelsea wanatarajiwa kuthibitisha kuwa mshambuliaji wa kimataifa Ufaransa Olivier Giroud, 32, amekubali kusalia katika klabu hiyo kwa mwaka mmoja mwingine. (London Evening Standard)

Meneja wa Ireland Kaskazini Michael O’Neill amaeibuka moja wa watu wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya umeneja iliyoachwa wazi West Brom. (Express and Star)

Antoine Griezmann na Olivier GiroudHaki miliki ya pichaEPA

Meneja mkuu wa Hertha Berlin Michael Preetz amefanya mazungumzo na mwenzake wa Liverpool Jurgen Klopp katika juhudi za kutafuta huduma za kiungo wa kati wa kimataifa wa Serbia Marko Grujic, 23, kwa mkopo wa mwaka mwingine tena. (Liverpool Echo)

Mlinzi mahiri wa zamani wa Brighton Bruno, 38, anasomea kozi ya ukufunzi wa Uefa mjini Belfast. (Argus)

Chanzo BBC.

By ALLY JUMA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents