Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatano hii, Fellaini, Higuain, Eriksen, Ozil, Morata, Carrasco na wengine sokoni

Manchester United wamekubali kumuuza kiungo wao wa kati, mbelgiji Marouane Fellaini, 31, kwa kima cha euro milioni 15 mwezi huu.

Tayari vilabu vya AC Milan, Porto na Guangzhou Evergrande ya Uchina vimeonesha nia ya kutaka kumsajili. (Mirror)

Chelsea wanatarajiwa kuendelea mbeli na mpango wao wa kumsajili mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, ambaye yuko kwa mkopo AC Milan, kufikia mwisho wa wiki hii. (Telegraph)

Meneja wa AC Milan Gennaro Gattuso amesema kuwa Higuain hajamwambia kuwa anataka kuondoka klabu hiyo. (Evening Standard)

Christian Eriksen, 26,huenda akatia saini mkataba mpya na Tottenham, wakati ambapo Real Madrid pia inapigiwa upatu kumsajili kiungo huyo wa kati raia wa Denmark. (AS)

Arsenal wanataka winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco, 25, kujiunga nao lakini hawana uwezo wa kumsaini kiungo huyo kutoka klabu ya Dalian Yifang ya Uchina.

Gunners wanaweza kufanya hivyo endapo watamuuza kiungo wao wa kati Mesut Ozil. (Fox Sports Asia)

Arsenal watalazimika kupunguza malipo ya Ozil ya euro 350,000 kwa wiki kumuachia nyota huyo huku kukiwa na uwezekano wake kujiunga na Inter Milan kwa mkopo. (Mirror)

Barcelona wanapania kumsaini mshambuliaji mpya na kuna tetesi kuwa huenda wamnunua Cristhian Stuani, 32, wa Girona huku wakiwalenga washambuliaji wengine kama Fernando Llorente, 33, wa Tottenham na Olivier Giroud, 32, na Alvaro Morata, 26, kutoka Chelsea. (Marca)

Azma ya mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata ya kutaka kuhamia Atletico Madrid huenda ikafifia kwa sababu klabu hiyo ya Uhispania inataka kumsajili Morata kwa mkopo hadi kmwisho wa msimu huu. (Mail)

Leicester huenda wanamuajiri meneja wa Celtic Brendan Rodgers kuchukua nafasi ya meneja wao wa sasa Claude Puel. (Sun)

West Ham wamekataa ofa ya euro milioni 8.9 kutoka kwa Fiorentina ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Equatorial Guinea Pedro Obiang. (Sky Sports)

Arsenal wanamfuatilia kwa makini kiungo wa kati wa Colombia James Rodriguez na huenda wakalipa euro milioni 3 kwa Real Madrid ili kubadilisha miezi sita ya mwisho ya mkataba wake wa kuichezea kwa mkopo Bayern Munich kwa miaka miwili.(Mail)

Bournemouth wanatarajiwa kuweka dau la euro milioni 15 kumnunua beki wa kati wa Brentford na Wales Chris Mepham, 21, ili kumzuia asijiunge na Southampton. (Sun)

Chelsea wameongeza ofa ya euro milioni 36 kumnunua kiungo wa kati wa Argentina Leandro Paredes, 24, kutoka Zenit St Petersburg ya Urusi.(Star)

Mshambuliaji wa West Ham na Mexico Javier Hernandez, 30, anataka kujiunga na Valencia, lakini Hammers huenda wasimuachilie hadi wapate mchezaji atakayechukua nafasi yake. (Guardian)

Manchester United wameanza mazungumzo na Tromso kumhusu Isak Hansen-Aaroen ili kuzima azma ya Everton na Liverpool kumnunua. (Aftenposten, via Manchester Evening News)

Manchester City hawana mpango wa mpango wa kumnunua Isco ambaye ni kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania. (ESPN)

Kipa wa Real Madrid Kiko Casilla, 32, alikosa kufika mazoezini siku ya Juma nne na badala yake kusafiri England kufanya vipimo vya kimatibabu na klabu ya Leeds United. (AS)

Newcastle hawajaweka dau mpya ya kumnunua kiungo wa kati wa Paraguay Miguel Almiron, 24, kutoka MLS Atlanta United tangu ufa yao ya kwanza kukataliwa mwezi Desemba mwaka jana. (Chronicle)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents