Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatatu hii, Griezmann, Sarri, Felix, Rodriguez, Richarlison na wengine sokoni

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid Antoine Griezmann anajuta kutojiunga na Barcelona msimu uliopita na sasa anatamani kujiunga na klabu hiyo ya Nou Camp. (L’Equipe – in French). Lakini licha ya kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amesema yuko tayari kujiunga na klabu nyengine za Ulaya ikiwemo Barcelona, klabu hiyo ya Catalan haina haja naye.. (ESPN)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich huenda akatumia likizo ya kimataifa kumfuta kazi kocha Maurizio Sarri baada ya kulazwa na Everton siku ya Jumapili. (Express).

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich huenda akatumia likizo ya kimataifa kumfuta kazi kocha Maurizio Sarri

Kiungo wa kati wa Bayern na Colombia James Rodriguez, 27, hataki kusalia mjini Munich zaidi ya kipindi chake cha mkopo kutoka Real Madrid, kinachoisha mwisho wa msimu huu. (Marca)

Kiungo wa kati wa Bayern na Colombia James Rodriguez, 27, hataki kusalia mjini Munich zaidi ya kipindi chake cha mkopo kutoka Real Madrid,

AC Milan huenda ikazuiwa na thamani ya Everton ya Yuro milioni 70 za mchezaji wa klabu hiyo mwenye umri wa miaka 21 raia wa Brazil Richarlison. (Calciomercato)

Mshambuliaji wa klabu ya Benfica Joao Felix anasema kuwa anafurahia kuwa katika klabu hiyo , licha ya hamu kutoka kwa klabu za Manchester United na Chelsea. Liverpool awali walikuwa wametoa ofa ya £61m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 iliokataliwa. (Marca – in Spanish)

Liverpool wamewasiliana na Benfica kuhusu uwezekano wa kuvunja rekodi ya dunia katika usajili wa beki wa kati wa Ureno Francisco Reis Ferreira, 21. (Record, via Metro)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ataendelea kuifunza timu hiyo kwa muda mrefu baada ya nahodha wa zamani wa Ujerumani Franz Beckenbauer kusema kuwa huenda akaifunza Bayern Munich. (Liverpool Echo)

Kituo cha reli cha White Hart Lane kinatarajiwa kupewa jina la Tottenham Hotspur, huku majadiliano na umma yakiendelea. (Guardian). Mwenyekiti wa klabu ya Spurs Daniel Levy anasema kuwa dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu huu halitaathiriwa na thamani ya uwanja mpya. (ESPN)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ataendelea kuifunza timu hiyo kwa muda mrefu baada ya nahodha wa zamani wa Ujerumani Franz Beckenbauer kusema kuwa huenda akaifunza Bayern Munich. (Liverpool Echo)

Arsenal itafikiria kumsajili mchezaji wake wa zamani Marc Overmars kuwa mkurugenzi wa kiufundi baada ya kumkosa Monchi waliyekuwa wakimlenga sana ambaye ameamua kurudi katika klabu ya Sevilla baada ya kuondoka Roma. (Telegraph)

Juventus imejiandaa kumpatia ofa Alexis Sanchez,

Juventus imejiandaa kumpatia ofa Alexis Sanchez, 30, ili kuondoka katika klabu ya Manchester United, lakini mchezaji huyo wa Chile atalazimika kupunguza mshahara wake (Calciomercato)

Inter Milan wameiambia Real Madrid kwamba wanataka Yuro milioni 80 kwa mchezaji wa Argentina, 26, Mauro Icardi, ambaye hajaichezea klabu hiyo ya Serie A tangu alipovuliwa unahodha wa klabu hiyo mwezi uliopita . (AS)

Newcastle iko tayari kufanikisha mpango wa kumuongezea muda kocha wake Rafael Benitez haraka iwezekanavyo kufuatia wasiwasi kuhusu majina mapya ya mameneja wanaotarajiwa kumrithi kocha huyo mbali na raia huyo wa Uhispania kuhusishwa na vilabu vingine. (Chronicle)

Newcastle iko tayari kufanikisha mpango wa kumuongezea muda kocha wake Rafael Benitez

Arsenal, West Ham na Inter Milan wana hamu ya kumsajili beki wa kulia wa klabu ya Manchester United Antonio Valencia wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu huu, kulingana na babake na ajenti wa mchezaji huyo raia wa Ecuador mwenye umri wa miaka 33. (El Universo, via Sky Sports)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents