Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatatu hii, Guardiola, Gundogan, Jokanovic, Mbappe na wengine sokoni

Pep Guardiola, ambaye hivi karibuni alihusishwa na Juventus, amewaambia marafiki zake kuwa yuko tayari kusalia Manchester City kwa miaka minne ijayo. (Telegraph). Guardiola ametilia shaka hatima ya kiungo wa kati, Ilkay Gundogan katika klabu ya Manchester City baada kufichua kuwa mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 28 huenda usiongezwe. (Mirror)

West Brom itafanya mazungumzo zaidi na meneja wa zamani wa Fulham, Slavisa Jokanovic siku ya Jumatatu wanapoendelea na kampeini ya kumsaka kocha mpya baada ya Darren Moore kufutwa kazi. (Telegraph). Tottenham na Arsenal huenda wakamshindania kiungo wa kati wa na Villarreal, Pablo Fornals, 23.

Gunners huenda wakmuuza Mesut Ozil kabla ya kuchukua hatua hiyo. (Express). Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe, 20, ambaye amehusishwa na Real Madrid, amepuuzilia mbali tetesi kwamba huenda akaondoka Paris St-Germain msimu ujao. (Squawka)

Manchester City inamfuatilia kiungo wa kati wa Lyon, Tanguy Ndombele kwa lengo la kumnunua kiungo huyo wa miaka 22 -msumu huu wa joto. Ndombele, mia anafutiliwa na Tottenham, Manchester United na Juventus. (Express)

Tottenham huenda ikamnunua kiungo wa kimataifa wa Argentina, Giovani Lo Celso, ambaye amefunga mabao 12 akiwa Real Betis kwa mkopo kutoka Paris St-Germain msimu huu, ikiwa Christian Eriksen, 27, ataondoka klabu hiyo kujiunga na a Real Madrid. (Talksport)

Hatahivyo Betis inaonekana kunda imefanya uamuzi wa kumsaini Lo Celso -ambaye pia analengwa na Real Madrid – kwa mkataba wa kudumu wa euro milioni 21.5 msimu wa joto. (Marca

Meneja wa muda wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekanusha madai kuwa kipa wao David de Gea aliathiriwa na mzozo unaoendelea kuhusiana na mkataba wake wakati wa mechi yao dhidi ya Arsenal ambapo walifungwa mabao 2-0. (Evening Standard)

Celtic inapania kumsaini mlinzi wa Chelsea, Tomas Kalas, 25, amabye anachezea Bristol City kwa mkopo. (Daily Record)

Kilmarnock imetoa ofa ya awali kabla ya kuingia mkataba na kiungo wao wa kati wa zamani, Craig Bryson, 32, wa Derby ambaye mkataba wake unakamilika mwisho wa msimu huu. (Express)

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amemkosoa Eden Hazard kwa kutocheza vizuri licha ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Wolves. (Talksport).

Chelsea imemweka meneja wa Wolves Nuno Espirito Santo katika orodha yao uhamisho wa mameneja. (Star)

Mlizi nguli Sergio Ramos, 32, ana mpango wa kuondoka Real Madrid msimu huu ikiwa klabu hiyo itamuajiri meneja wao wa zamani Jose Mourinho. (Daily Mail)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents