Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatatu hii, Maguire, Keita, Verane, Barella, Bale, de Ligt na wengine sokoni

Manchester United wametaarifiwa kuwa itawalazimu kuvunja rekodi ya usajili ili kumnasa mlinzi raia wa Uingereza Harry Maguire, 26, anayekipiga katika klabu ya Leicester. (Star). Liverpool wanatazamia kumruhusu kiungo Naby Keita, 24, kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu na watakubali kula hasara katika thamani ya mchezaji huyo raia wa Guinea. (Sun)

Klabu za Manchester United, Arsenal na Tottenham zinamnyemelea beki kinda raia wa Denmark anayechezea klabu ya Sampdoria ya Italia Joachim Andersen, 22. (CalcioMercato).

Liverpool watamkosa beki wa kati raia wa Uholanzi anayecheza katika klabu ya Ajax Matthijs de Ligt wakati huu ambapo rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu yupo safarini kwenda kufanikisha makubaliano ya kumnasa mlinzi huyo mwenye miaka 19. (Sun)

Matthijs de Ligt (kushoto) sasa anatarajiwa kufikia makubaliano ya kujiunga na Barcelona baada ya kuwaniwa vikali pia na klabu za Juventus, Man City na Liverpool

Arsenal wanapanga kumsajili kiungo wa klabu ya Charlton Athletic Joe Aribo, 22, mwishoni mwa msimu. (Mirror)

Gareth Bale atakaribishwa tena kwa bashasha katika klabu ya Tottenham iwapo winga huyo raia wa Wales mwenye miaka 29 ataamua kuondoka katika klabu yake ya sasa Real Madrid na kurejea London, amesema beki wa Spurs Ben Davies. (Goal)

Bale ameripotiwa kutokuwa na maisha ya furaha ndani ya klabu yake ya Real Madrid

Liverpool wameingia katika kinyang’anyiro cha kumnyemelea beki wa Inter Milan na raia wa Slovakia Milan Skriniar, 24. (TeamTalk)

Juventus wanatarajiwa kumsaka beki wa Real Madrid Mfaransa Raphael Varane , 25, baada ya mlinzi huyo kuiambia klabu yake kuwa anataka kuihama. (Football Italia)

Verane (kulia) akipambana na Leo Messi kwenye mchezo wa el classico .

Everton na Newcastle ni miongoni mwa klabu za Ligi ya Primia ambazo zinamfuatilia beki wa kushoto wa klabu ya Olympiakos Leonardo Koutris. Leicester na West Ham pia wanamnyemelea Mgiriki huyo mwenye miaka 23. (TeamTalk)

Maskauti wa Arsenal walikuwa uwanjani wakimtathmini kiungo wa klabu ya Cagliari Nicolo Barella, 22, akifunga goli lake la kwanza kwa timu ya taifa ya Italia katika mchezo dhidi ya Ufini. (Metro)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents